Health&Food

Zijue Sababu au nyenzo za kukufanya wewe upate afya bora

on

Uwe na uwezo wa kupata na  kula chakula sahihi bora na cha kutosha

Jamii nyingi zinaweza kupata chakula ila changamoto ni kwamba mara nyingi hupata chakula cha aina moja tuu mfano wamasai huweza kula sana nyama, maziwa kwa sababu ndio chakula kilichopo kwao, lazima uweze kupata chakula tofauti tofauti mfano matunda, nyama , mboga mboga pia nafaka hii itakusaidia wewe kuweza kuwa na uwiano katika mlo wako wa siku,wiki hadi mwenzi. hii itakusaidia wewe kuweza kusimamia na kujenga afya yako.

Hamu ya kula

Hapa nazungumzia hali ya kupenda kula bila kulazimisha au kulazimishwa na mtu, pale ambapo mtu anaweza kupatwa na magonjwa ambayo yanaweza kushusha hamu ya kula humfanya kukataa kula hivyo basi mwili wake unadhoofika pia hata dawa ambazo hutumiwa kwa ajili ya kutibu maradhi mbalimbali husababisha pia hamu ya kula ipungue.

Uwezo wa kutafuna na kumeza

Binadamu anaweza akawa na hamu ya kula pamoja na uwezo wa kupata chakula bora ila akajikuta uwezo wake wa kutafuna chakula ni mdogo hii itamfanya yeye kuchagua vyakula na kupenda kula vyakula vya kimiminika pia kama hawezi kumeza pia itamfanya yeye kupewa vya kula vya kumiminika, magojwa kama kansa ya koromeo la chakula, kansa ya tumbo na matatizo mengine yanayopelekea mtu kushindwa kumeza chakula pia magonjwa ya kinywani kama vile fizi kuuma au meno kuuma na kutisika yote haya husababisha afya ya mtu kuzorota.

Uwezo wa kumeng’enyeka na kunyonya chakula

Baada ya chakula kutafunwa na kumezwa kwenda kwenye tumbo kinachofuata ni mmeng’enyo wa chakula hicho ili kiweze kuwa laini zaidi kisha kiingie ndani ya misuli na mishipa ya damu tayari kwa kutumika katika kuupa mwili nguvu na kuufanya ukue pale ambapo mwili unashindwa kufanya hivi kinachotokea ni kwamba unachokila hakiendi panapohusika hivyo zile virutubisho vya mwili kushindwa kutumika.

Uwezo wa kutumia chakula katika seli za mwili na mifumo mingine ya mwili pia uwezo wa kutoa taka mwili nje baada ya mmeng’enyo wa chakula kufanyika

Vyote hivi huweza kupelekea mtu kuwa na afya bora ukishindwa kukojoa au kutoa choo nje hukusababisha wewe kutokuwa na afya bora pia lazima virutubisho vyako ambavyo umezila katika chakula viweze kufika katika seli zako ili kuziwezesha ziwe na uhai na nguvu ya kupambana na maradhi pamoja na ukuaji wa sehemu mbali mbali za mwili.

Mazoezi

Haya huweza kufanya mmeng’enyo wa chakula kufanyika vizuri pia kuzuia baadhi ya magonjwa yatokanayo na chakula kama kisukari na shinikizo la damu kutokutokea kuna aina mbili ya mazoezi mazoezi ambayo hutumia hewa ya oxygen mfano kukimbia, kupiga push up kuruka kamba pia kuna mazoezi ambayo hayatumii hewa ya oxygen kama kubeba vyuma n.k, Mazoezi husababisha mtu kutokupata tatizo la tumbo kujaa gesi kwa sababu chakula humeng’enywa vyema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *