Health&Food

Zijiue chanjo ambazo hupewa mtoto wa chini ya miaka mitano

on

 Watoto wa chini ya miaka mitano ni watoto ambayo huwa na kinga ndogo sana ya mwili hivyo kuwafanya wao wawe katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali. Watoto hawa hucheza na kula vitu mbalimbali hivyo ni rahisi kupata maradhi ya kuambukizwa hivyo basi baada ya mtoto kuzaliwa kuna chanjo ambazo anapaswa kuchomwa ili kumzuia yeye alipate maradhi hatari kama kifua kikuu, kupooza na homa ya ini na mengiine.
  • BCG;
hii ni chanjo ambayo huchomwa bega la kushoto mara baada ya mtoto kuzaliwa. dozi yake ni 0.5mls humkinga mtoto na ugonjwa wa KUFUA KIKUU pale akiwa mdogo.
  • POLIO
Hii ni chanjo ambayo hutolewa mara tatu kwa mtoto. mara ya kwanza ni pale ambapo mtoto anazaliwa, mara ya pili ni wiki nne baada ya kupewa ile ya kwanza na ya tatu ni baada ya wiki nne baada ya kupewa ile ya pii. Dozi yake ni matone mawili unampa kwa njia ya kunjwa. Hii husaidia kumkinga mtoto kwa ugonjwa wa KUPOOZA.
  • DTP(PENTAVILLENT)
Hii huchomwa katika paja la mtoto mara tatu wiki nne baada ya kuzaliwa alafu wiki nne anapewa ya pili na mwisho baada ya wiki nne anapewa ya mwisho. Dozi yake ni 0.5mls hii huzuia magonjwa kama DONDA KOO, KIFADURO, HOMA YA INNI, TETANUS NA KUPOOZA.
  • PCV 13
Hii huchomwa pia kwenye paja na huolewa mara tatu kwa utofauti wa muda kama hizo apo DTP. Dozi yake ni 0.5mls hii husaidia kumkinga mtoto na ugonjwa wa NIMONIA.
  • ROTA VIRUS
hii ni chanjo ambayo hutolewa mara mbili kwa mtoto ya kwanza ni wiki nne baada ya mtoto kuzaliwa na ya pili ni wiki nne baada ya kupewa ya kwanza. Dozi yake ni matone mawili na humkinga mtoto na ugonjwa wa kuharisha.
  • CHANJO YA SURUA
Hii hutolewa  mara moja tu kwa kuchomwa kwenye bega baada mienzi sita baada ya mtoto kuzaliwa, humkinga mtoto na ugonjwa wa SURUA.
                                                   mwisho

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *