LifeStyle

Yafahamu mambo muhimu 4 ya tabia yanayothibitisha jinsi tabia inaweza kukufanya ufanikiwe au ufeli

on

Tabia ni kitu ambacho kinajengeka kwa kuangalia watu unaoishi nao pamoja na mazingira yanayokuzunguka mafanikio ya mtu mara nyingi huchangiwa na tabia yake, Tunapozungumzia mafanikio ya mtu tunayaangalia katika nyanja mbalimbali kama kimapato, kimahusiano na mambo mengine . Unapokuwa na tabia chanja katika maisha yako hukupa fursa ya kuweza kufanya mambo ambayo yapo katika malengo yako kisha kuweza kuyafanikisha ila ukiwa na tabia hasi utaandamwa na mambo hasi utashindwa kusimamia malengo yako. Tabia hufanya mambo yafuatayo;-

Hutuongoza sisi ;- Mara nyingi mtu hutenda jambo kulingana wewe ulivyo , unachokiwaza na unachokisema  tabia hukufanya utende vitu vizuri au vibaya tabia hukuongoza wewe katika kufanya mambo ambayo baadaye utakuja kuyajutia au utakuja kuyafurahia siku za mbeleni.

Hutuamasisha;-  Mfano mtu akiwa na tabia ya kunywa pombe au kutumia madawa ya kulevya tabia hiyo humpelekea yeye kutaka kutumia hivyo vitu pindi ambapo anakosa pia pale ambapo mtu anakuwa na tabia labda ya kusoma au kucheza au kufanya kazi kwa bidii lazima akiwa hajafanya hicho kitu moyo wake au nafsi yake inasononeka kwa hiyo akitenda hivyo hufurahi sana . asilimia kama 95 ya vitu ambavyo tunatenda husababishwa na huamasishwa na tabia ambayo tumejijengea.

 

 

Hukufanya wewe ufanye chaguzi;- tabia hukufanya wewe ufanye chaguzi ya sehemu ambayo utaishi kulingana na ulivyo kuweza kufanya mambo yako vyema pia hukufanya wewe kukubali kuishi na tabaka fulani la watu na kukataa tabaka fulani la watu kwa hiyo tabia hukufanya wewe kutembea na watu wabaya au kutembea na watu wazuri wenye kupenda mafanikio. jua kwamba chaguzi hutengeneza tabia na tabia hutengeneza chaguzi.

Hukubadilisha;- Tabia hukujengea maozoea fulani ambayo pengine mwanzoni hukuwa nayo mfano tabia inaweza kukuhamisha kutoka kwenye kutenda mambo ya kimsingi na yenye tija katika maisha yako yenye uwezo wa kukufanya wewe kutimiza malengo na kuanza kukufanya wewe kuachana na mipango hiyo kisha kudumbukia katika mambo yatakayokuporomosha kimaisha, Tabia huleta mabadiliko na mabadiliko huleta tabia.

 

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *