Uncategorized

WCB Wasafi wananihitaji ila sipo tayari – Z Anto

on

Msanii Z Anto ambaye aliwahi kutamba na ngoma kibao kali kama ‘Binti
kiziwi, Mpenzi jini, Kisiwa Cha Malavidavi amefunguka na kusema kuwa
mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji na kuhitaji
kufanya naye kazi.

Z Anto

Akiongea
kwenye kipindi cha Planet Bongo Z Anto amesema alipata ofa kujiunga na
WCB Wasafi lakini yeye mwenyewe anadai anatamani kufanya kazi nje ya WCB
Wasafi hivyo hawezi kujiunga nao.

“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka
saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo
sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati
ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha
kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na
maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi
natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip
Top Connection” alisema Z Anto 

Msanii huyo alitoa sababu kubwa yeye kutamani kufanya kazi nje ya
Wasafi akidai tayari chini ya ‘label’ hiyo kuna mafahari hivyo hadhani
kama mafahari wawili wanaweza kupatana au kwendana 

“Sisi ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya
kazi sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo
mengi mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda
kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi
muda si mrefu’ alisema Z Anto.

CHANZO: EATV.TV

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *