Uncategorized

VYAKULA NA VINYWAJI VINAVYOWEZA KUKULETEA MADHARA KATIKA AFYA YAKO PALE UKIZIDISHA ULAJI WAKE.

on

Katika maisha ya sasa inaonekana kwamba vyakula vingi ambavyo huwa watu wanakula vinamadhara sana na hii ni kwa sababu vyakula na vinywaji vingi huwa vimewekwa na kurutubishwa na kemikali. Vifuatavyo ni vyakula na vinywaji ambavyo vinamadhara kwa afya;

  


VYAKULA VYENYE SUKARI;

Hivi ni kama sukari, ugali kiujumla vile vyakula vitamu sana katika mwili wa binabamu kuna kiungo kinaitwa kongosha ambacho hutoa homoni ambayo huusika na maswala ya kuhakikisha kiwango cha sukari  kinakuwa sawa kwa hiyo pale ambapo unatumia sana sukari huku hufanyi mazoezi au kazi ngumu hufanya kongosho lizidiwe na kuruhusu sukari kuwa nyingi ndani ya damu na hapa ndipo mtu anapata ugonjwa wa kisukari.


NYAMA ZA MAFUTA;

Hizi husababisha madhara makubwa katika moyo na mishipa ya damu kwa sababu tabia ya haya mafuta huwa yanaganda kwa hiyo yakifika ndani ya mishipa ya damu au moyo huwa yanaganda katika kuta zake na kusababisha kuwa miembanba na hivyo mtu kupata shinikizo la damu na moyo kushindwa kufanya kazi kawaida.
POMBE; 


Hii huwa na chemikali kubwa au sumu na tunavyofahamu kazi ya ini ni kuchuja sumu zote zinazoingia katika mwili kwa hiyo pale ambapo unatumia   kupita kiasi husababisha ini kuchoka na kushindwa kufanya kazi na kupelekea sumu kuzunguka mwilini na kuleta madhara kama tumbo kujaa maji, figo kushindwa kufanya kazi.

VYAKULA VYA KIWANDANI;


Hivi ni vyakula vya makopo kutokana na kemikali zinazowekwa huko ili kusindika chakula hicho kisiaribike huweza kusababusha magonjwa ya kansa ya tumbo na vidonda vya tumbo.

vingine ni kama mboga, matunda ambayo yameoteshwa na kunyunyuziwa kemikali hii pia hupelekea magonjwa ya satratani.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *