Uncategorized

VIKWAZO DHIDI YA USINGIZI MURUA NA SULUHU ZAKE

on

Usingizi ni moja kati ya vitu muhmu kwa afya ya binadamu. Kukosa
usingizi ipasavyo (masaa 6-8) hupelekea matatizo kama uchovu siku
inayofuata, kusinzia siku inayofuata, kupungua uzito, kupungua kinga ya
mwili n.k. Kuna imani potofu ya kwamba watoto ndio wanaopaswa tuu kulala
muda fasaha.

Kwa kuwa watu wengi hawapo makini katika kuangalia mienendo ya maisha
yao, hawawezi kujua sababu zinazopelekea matatizo hayo, hivyo kukosa
sululuhu ya kudumu. Zifuatazo ni sababu zinazopekea ukosefu wa usingizi,
baada ya kuzijua itakuwa rahisi kwa mtu kukabiliana na changamoto.

Kula chakula kingi muda mchache kabla ya kulala.

Kula chakula kingi, hususani nafaka, muda mfupi kabla ya kulala hufanya
mwili utumie nishati nyingi katika kumeng’enya chakula, hivyo kuvuruga
utaratibu wa nishati wa mwili. Pia kunywa maji kabla ya kulala humfanya
kuamka usiku ili kujisaidia, hivyo kubadili utaratibu wa usingizi.
Mtu anapaswa kula chakula chepesi na maji kidogo angalau nusu saa kabla ya kulala.

Kulala mazingira duni.

Kulala katika mazingira yanayokinzana na utu wa mtu huvuruga utaratibu
wa mwili. Mazingira kama; chumba chenye mwanga mkali, chumba chenye joto
au baridi kali, kulala kwenye kelele, kulala kwenye godoro laini au
gumu sana, chumba kisicho na hewa safi ya kutosha n.k humfanya mtu
kukosa usingizi.

Kubadili mfumo wa maisha.

Kubadili mfumo wa maisha na ambao ulikuwa umezoelewa na mwili hutatiza
usingizi. Kwa mfano; kumpoteza ndugu au rafiki wa karibu, kuanza kazi
mpya, kufanya kazi ngumu, kuingia kwenye ndoa, kuwa na msongo mawazo n.k
huwafanya watu wengi kukosa usingizi.
Hali hii huchukua siku chache, ikiwa kama ukosefu wa usingizi itachukua muda mrefu, mtu anapaswa kufanya tahtmini ya kina.

Mazingira duni ya kijamii.

Mazingira duni ya kijamii kama; kulala zaidi ya mtu mmoja kwenye kitanda
kimoja, kulala na mtu msumbufu hususani mtoto mdogo, kulala chumba
kimoja na mtu anayekoroma, kulala na mtu anayesumbua usiku, kulala
chumba chenye wadudu kama chawa, kunguni, viroboto n.k.
Mazingira haya yanasababishwa na umasikini wa kipato.

Matumizi ya madawa.

Kuna aina nyingi sana ya madawa ya hosptalini ambayo, pamoja na kutibu
au kupunguza maumivu, hupelekea kukosekana kwa usingizi. Madawa hayo ni
kama madawa ya kupunguza maumivu, kupunguza mawazo, madawa ya usingizi
n.k.
Mtu anapaswa kusoma maelekezo au kupata ushauri wa daktari kabla ya
kutumia dawa yoyote ile ili apate kujua madhara yake na jinsi ya
kuyakabili.

Matumizi ya vinywaji baridi na sigara muda mchache kabla ya kulala.

Vinywaji baridi vina kokaini, chai au kahawa ambayo huongeza msukumo wa
damu. Matumizi ya vinywaji hivyo kabla ya kulala kukatiza usingizi. Kwa
upande wa sigara, ikilinganishwa na watu wasiovuta sigara, watu
wanaovuta sigara hukawia kupata usingizi, hivyo, kupata masaa machache
ya kulala.
Kuna watu wamezoea kunywa pombe ndipo wapate usingizi, watu hawa ni
watumwa wa pombe na wengi wao hutumia pombe kali, baada ya muda, pombe
haitoweza kumsabishia usingizi kabiasa au akiwa hana hela ya kununua
pombe mtu huyo hatoweza kulala.

Kwa kiasi kikubwa, sababu za ukosefu wa usingizi zipo chini ya uwezo wa
binadamu, hivyo, mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla inapaswa
kutengeneza mazingira yanayopekekea usingizi murua, mafanikio ya mtu
katika kazi za kujiletea maendeleo, hutegemea, pamoja na mambo mengine,
kiasi cha mapumziko anayopata kila siku kupitia usingizi.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *