Uncategorized

Utafiti: Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua kwa umri

on

Kitambi ni hali ya kiafya ya mtu mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa kiasi kikubwa. Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo kubwa la kiafya duniani. Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.
Katika mawazo ya kizamani na hata sasa katika baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni tajiri.
Tatizo la unene na vitambi litazidi kuongezeka ikiwa serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za dharura na mipango madhubuti kulikabili.
Vitambi hupunguza maisha ya watu wenye hali hiyo ya afya, hivyo kusababisha upotevu wa rasilimali watu. Ili kuepukana na athari hiyo watu wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi na milo yao. Wengi wana muda mchache sana wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na vitambi.
Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya njema.
Watu wengi, hasa vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari na si mbogamboga na matunda. Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka kila sehemu.
Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *