Health&Food

Ufahamu ugonjwawa Typhoid (maana,dalili na matibabu )

on

Huu ni ungojwa ambao husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhimurium. Bakteria hawa huishi  katika damu na sehemu ya utumbo ndani ya mwili wa binadamu. Bacteria hawa huambukizwa kwa kugusa moja kwa moja choo cha mtu ambaye tayari ameadhiriwa na ungojwa wa typhoid. Hakuna myanyama ambaye hubeba bacteria hawa kwa hiyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu.

Mgonjwa mmja kati ya wanne hupoteza maisha kama wamekosa matibu na kama wamepata matibabu wagonjwa 100 hupona na wanne huwa katika hali mbaya.Bacteria hawa huingia kwa njia ya mdogo kwa kula chakula kilicho na salmonella Typi, kunywa maji machafu na kula kitu bila kunawa mikono. Bacteria hawa huishi kwenye utumbo kwa binadamu kwa muda wa wiki 1 hadi mbili kisha hutumia mishipa midogo ya damu kwenda katika sehemu mbalimbali mwilini kisha kuanza kushambulia maeneo mbalimbali ya mwili.

Mgonjwa hupimwa choo,mkojo,damu na mfupa ili kutambua ugojwa huo.

Dalili zake ni hizi hapa

Dalili huanza siku 3 hadi 30 ambazo ni;-

 • Homa
 • Kuharisha
 • Tumbo kuuma
 • kutapika
 • Kuchanganyikiwa
 • kunya choo kigumu

Namna ya kujikinga na ugonjwa huu

 • kunywa maji safi na salama
 • Nawa mikono kabla ya kula
 • Nawa mikono baada ya kutoka chooni
 • Usipende kula vyakula vya mitaani
 • Hakikisha unakula matunda ambayo yameoshwa vizuri.

Matibabu ya ugonjwa huu

 • Dawa ambayo hutibu vizuri typoid ni Ciproflaxin dawa hii hupewa kulingana na ungonjwa ulivyokuathiri
 • kunywa maji kwa wingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *