Health&Food

Ufahamu ugonjwa wa Kichocho maana,dalili,sababu na tiba yake

on

Kichocho ni ugonjwa ambao husababishwa na  minyoo aina Schistosoma ambao huishi ndani konokono wa majini(flukes) . Inakadiriwa kuwa watu zaidi milioni 218 duniani walipewa kinga ya ugonjwa huo mwaka 2015. Kulingana na Shirika la Afya Duniani nchi 78 zinasemekana kuwa na maambukizi ya kichocho. Inasemekana kwamba alisimia 90 ya matibabu   ya ugonjwa huu hufanyika Africa hivyo kuonekana kwamba ugonjwa huu umekidhiri sana katika bara la Afrika,Asia na Amerika ya kusini. Mwaka 2014 ugonjwa ulisababisha vifo vya watu  200,000 duniani

Usaambaaji au maambuzi yanavyotokea

Wadudu hawa uingia kwenye mwili wa binadamu kwa kupitia ngozi pale ambapo mtu anaogelea au kutumia maji ambayo tayari yana watoto wa wadudu aina ya schistosoma baada ya kuishi kwenye konokono wa majini.

Baada ya hapo vijidudu hivyo huingia kwenye damu mwilini hukua vikiwa mwilini kisha kukaa kwenye mishipa ya damu na kuanza kutaga mayai baadhi ya mayai hutoka nje kwa njia ya haja kubwa au haja ndogo hivyo kama mayai ya wadudu hawa yatakutana na maji tena ambayo yana konokono wa majini ukuaji wake huendelea.  Mayai mengine huenda katika viungo vya mwili kisha kuharibu kazi zake pia upunguza uwezo wa mfumo wa kinga mwilini kupambana na magonjwa.

Mtu huambukizwa ugonjwa huu pale ambapo anaoga au kukanyaga maji ambayo tayari ameshachafuliwa na mkojo au haja kubwa ya mtu mwenye Kichocho. picha hapo chini inaonyesha jinsi ukuaji wa mdudu huyu unavyofanyika

 

Dalili za Kichocho

 1. Tumbo kuuma
 2. Kuharisha
 3. Kutapika
 4. kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu
 5. Kukojoa mkojo uliochanganyika na damu
 6. kupata maumivu wakati wa kujamiana
 7. kupata viumbe vingi katika sehemu ya uke
 8. Tni kuvimba
 9. Tumbo kuvimba

(Konokono wa majini ambao husababisha kichocho)

Mambo ya kijamii ambayo husababisha ugonjwa huu

 • Kutokuwa msafi
 • kuogelea
 • kuvua samaki
 • Tabia za kucheza sana sana kwa watoto wa shule
 • shughuli za umwagiliaji

Matibu 

 • Hupewa dawa ya kuuwa minyoo inayoitwa Praziquantel na kiasi cha dozi yake hutegemea na uumwaji wa mgojwa na umri , uzito pia.
 • Epuka kuogelea sehemu za mitoni,baharini au katika bwawa la kuogelea ambalo mazingira yake si mazuri
 • Hakikisha unaposikia haja kubwa au ndogo unaenda chooni

 

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *