Health&Food

TUKIWA WASAFI UNAWEZA KUEPUKA MAGONJWA YAFUATAYO

on

Kuharisha
Huu ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea(bacteria) ambao huenezwa na inzi. kwa hiyo kama tukihakikisha kwamba

  • choo kipo safi hakina uchafu
  • tunanawa mikono baada ya kutoka chooni
  • tunaosha vyombo mara baada ya kumaliza kula
  • Tunatunza vyombo vya kulia katika sehemu safi.
  • Pia tuoshe matunda kabla ya kula.
Malaria
Huu ni ugonjwa ambayo huenezwa na mbu wa kike aina ya anopheles. kwa hiyo ili kuepuka tuhakikishe kwamba
  • Tunafyeka nyasi ndefu ambazo zipo katika mazingira yetu.
  • Tunafukia madimbwi ambayo yanatwamisha maji katika maeneo yetu ya kuishi.
Kifua kikuu
 
Huu ni ugonjwa ambao huenzwa kwa njia ya hewa ili kuudhibiti inatakiwa;;;;
  • Kunywa maziwa fresh yaliyocheshwa na kuwekwa katika chombo safi.
  • Hakikisha nyumba yako inakuwa na madirisha makubwa na yakutosha ili kuruhusu hewa.
  • Usile nyumba moja na mifugo.
Trakoma
huu ni ugonjwa ambao huenzwa na inzi
 cha kufanya ni kama hapo kwa kuharisha ili kujikinga. Kumbuka kunawa uso mara baada ya kuamka.
Mashilingi na fangasi
Ili kujikinga hakikisha unafuta yafuatayo
Oga mara kwa mara
kata kucha zako mara kwa mara
Kausha miguu na vidole vyako baada ya kunawa au kuoga.
Usishirikiane vitu kama chana na sabuni

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *