Health&Food

Ufahamu ugonjwa wa shinikizo la damu na madhara yake.

on

SHINIKIZO LA DAMU NI NINI?

Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

shinikizo hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:
 1. Uvutaji sigara
 2. Unene na uzito kupita kiasi
 3. Unywaji wa pombe
 4. Upungufu wa madini ya potassium
 5. Upungufu wa vitamin D
 6. Umri mkubwa
 7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
 8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

Uanishaji wa shinikizo la damu

Presha ya kawaida <120 <80
Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110
Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.
Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).
Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili za shinikizo la damu:

 • Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
 • Kuchanganyikiwa,
 • Kizunguzungu,
 • Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
 • Kutoweza kuona vizuri au
 • Matukio ya kuzirai.
 • Uchovu/kujisikia kuchokachoka
 • Mapigo ya moyo kwenda haraka
 • Kutokuweza kuona vizuri
 • Damu kutoka puani
Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.
‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. Batmanghelidj’.
Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.
Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.
Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo ‘renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho ‘angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya ‘adreno’ kutoa homoni iitwayo ‘aldosteroni’ ambayo huzifanya figo kuishikiliachumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.
Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.
Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.
Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.
Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo ‘vasopressini’ hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.
Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.
Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).
Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.
Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.
Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.
Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.
Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.
Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;
 • Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
 • Shambulio la moyo (heart attack)
 • Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
 • Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
 • Kiharusi
 • Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
 • Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *