Uncategorized

SABABU ZA KIHAMASA 5 ZINAZOMFANYA MTU KUWA MJASIRIAMALI

on

1. Msukumo
huu wewe kama ni mtu ambaye unapenda kweli kuwa mjasiriamali lazima uwe na imani kwamba unachokifanya kitakuletea faida pia ukichukua bidii yako ya kufanya kazi ukajumlisha na msikumo wako wa kutenda kazi unapata mafanikio yako.

2. Kujitolea 

mojawapo ya tabia kubwa ya mjasiriamali ni hii kujitolea na kupenda kufanya maamuzi huru bila kunyimwa kitu chochote na mtu yeyote. penda kujitoa katika malengo yako hii ni kwa sababu ndio sehemu pekee unapotegemea na unapopenda kufanikiwa zaidi. Hata kama kipato chake ni kidogo wewe ongeza kiu ya kufanya kazi yako.

3. Jisikie unakubalika

pale ambapo unafanya kitu kisha unaona watu katika jamii yako wanaokuzunguka wanakikubali wewe mwenyewe unajisikia furaha sana kisha hakikisha pia kabla hujalala ukiwa kitandani tenga muda wa kujiuliza je wateja wangu wamefurahia huduma ya leo? kama hapana ongeza mbinu za utendaji ili kufankisha lengo lako.

4. Jikuze mwenyewe

hapa namanisha kwamba tambua kuwa huna mtu ambae anakusaidia katika biashara yako au kampuni yako hivyo basi cha kufanya ni kufanya kazi kwa moyo na kwa bidii ili kuitanua kampuni yako mwenyewe pia angalia madhaifu yako kisha yatatue mwenyewe kwa kutengeneza jibu au njia imara za kuyatatua. Usiweke wazo la kumtegemea mtu.

5. Jiendeshe mwenyewe

Hii inamaana kwamba usipende kila kitu mtu anakuambia kiwe chanya kwako mara nyingi wajasiriamali huamini ubongo wao umewaza nini kuhusu kampuni yake au biashara yake so cha msingi ni wewe kujisikia kama bosi anayeshaurika hivyo utaweza kupanga na wenzako na kufikisha kampuni yako mahali kunakohitajika

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *