Uncategorized

ROMY JONES AMBAYE NI MENEJA TOUR WA DIAMOND NA HARAKATI ZAKE ZA KIMAISHA.

on

Akihojiwa katika kipindi cha SPORAH SHOW 

Romy ambaye ni TOUR MANGER wa Diamond, DJ namba mbili wa Diamond  amesema kwamba…… 

amelelewa tu na mama yake na pia amezaliwa wakati baba akiwa ameaga dunia. mama yake ni mfanyabiashara wa nje pia kaka yake anaishi nje  Africa ya kusini na yeye anaishi pamoja na Diamond na dada yake Diamond na mama yake katika nyumba moja. Mipango yake ni kufingua klabu na kuwa DJ kabisa.

Amekuwa pamoja na Diamond platnumz mama yake Romy ni mdogo ake na mama yake Diamond. Baba yake alifariki na kuwafanya wahamie karibu na nyumbani na Diamond. Wamesoma shule moja na Diamond poa wameishi  pamoja na Diamond. wakiwa shule ya msingi mama yake diamond alikuwa akiwachukuwa na kuwapeleka katika talent shows kwa sababu mama yake diamond alikuwa anapenda mziki sana.

Romy anasema kwamba alikuwa anapenda kutangaza na kuimba  alikuwa anapenda kurudia sana jinsi watangazaji wanatamgaza. Ilifika kipindi ambacho akikaa katika mziki alafu ukiisha anatangaza kama mtangazaji.

Adam Mchomvu ambaye ni rafiki yake alimwambia kwamba anakipaji cha kutangaza na akamwambia arekodi DEMO alafu azungumzie chochote then ampe ili aipeleke Ofisini Clouds Fm. Baada ya kutengeneza Mchomvu alimwambia apeleke DEMO Ijumaa kama bahati aliitwa kazini rasmi Jumatatu ya wiki iliyofuata na kuanza kazi Clouds Fm rasmi. 

Kwa kipindi hicho diamond ndio anaparangana na kutoka yeye Romy ndio alikuwa anamsaidia kwa kujitahidi kupambana na kuchukua uamuzi wa kumwambia Mchumvu kuwa anadogo wake anaimba ambeye ni Diamond.

Alichukua nyimbo ya diamond Jisachi na kuipeleka Clouds Fm na kumwomba mchomvu  ipigwe pigwe. Meneja wa kwanza aliwakacha baada ya kuona kwamba Diamond hapati mafanikio katika muziki. DIamond alitoa KAMWAMBIE ambayo Romy alikuwa akiipiga nyimbo hiyo mara kwa mara AIRTIME ili chali wake apate kutambulika kimuziki.

Diamond alitoa MBAGALA na ndiyo nyimbo ambayo ROMY anasema kwamba ilimtambulisha sana katika muziki hapa bongo. Diamond alipiga show ya kwanza Fiesta Romy hakuamini. ROMY anasema kwamba huwa mara nyingi anamshauri diamond ili asije potea.

challenge anazopata ni kwamba kuwakataza watu wasiongee na diamond mahala ambako hawaruhusu maongezi au kupiga picha na watu kumtext kwamba anaringa kwa sababu ya Diamond. kingine ni kuhusu Collabo anasema kwa sasa wamefocus collabo za Africa na Magharibi na pale anawanyima wasanii wa hapa huwa inatokea chuki za hapa na pale.

Anasema kwamba interview huwa wanazifanya kama zinaumuhimu hasahasa zile ambazo zinaelezea show ambayo wanaenda fanya. Anasema kwamba Diamond ni mtu ambaye anaheshimu wakubwa sana na pia anapenda kufikiri kabla ya kutenda na pia anajishusha kadri siku zinaenda na huwa anaenda na kulike picha za watu wakawaida ndani ya mitandao ya kijamii.

Anasema mara nyingi huwa wanagombana wakati wa kazi na mama yake Diamond huwa anawapatanisha. Pia wanagombana ila baada ya muda wanapatana wenyewe. Romy anasema anaye mpenzi lakini hapendi kuweka mapenzi yake katika uwazi. Anasema madhara yake ni kwamba mkiachana utaweka mwingine? pia anasema hapendi kujulikana sana. 

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *