Cellebs

Fahamu historia ya Salim Kikeke

on

NIMTANGAZAJI MAARUFU SANA KABLA YA UTANGAZAJI ALIWAHI KUCHIMBA MADINI MERERANI NA KUONA MAISHA MAGUMU AKAENDA SOMA DIPLOMA YA AGRICULTURE NA BAADAYE KUANZA KUTANGA MWAKA 2014 ALISHINDA TUZO YA MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA ZAIDI BONGO.

Akiongea na Michuzi TV  alisema kwamba…

Alisema kwamba siri ya mafanikio yake ni kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa pia kuamini kwamba anaweza kutimiza ndoto zake toka akiwa mdogo na bado hajatimiza kwa ujumla. Anasema mwanzani alipenda kusikiliza redio na kujiona kwamba anaweza kufanya hiyo kazi kisha kuweza kutangaza redio na baada ya Tv kuingia bongo nae alipata nafasi hiyo.

Watangazaji aliowapenda ni kama Dividi Wakati, Salim self  na Abdul Ngarawa hawa ndio watangazaji alipowasikia wakati huo aliona anaweza kuja kama wao. Kwa kimataifa ni Aly Sale, Tido muhando ambao walikuja baadaye kujuimuika naye katika utangazaji katika BBC Swahili.

Anasema kwamba hakusomea huandishi siku moja aliamka asubuhi na kwenda CHANNEL TEN na kuonana na  Mkurugenzi kuomba kazi mzee Godfrey Mgodo akamwambia  anataka kazi gani akasema uandishi wa habari na kumwambia kijana umekuja kuomba kazi huku unatafuna ubani na hakupewa kazi alikosa alijifunza kwamba huwezi omba kazi huku unatafuna ubani.

Alienda redio Tanzania na kuonana na mkurugenzi alikuwa ni Abdul Ngarawa na aliulizwa unauzoefu wowote akasema hapana hivyo akakosa kazi. Hakuishia hapo aliamua kwenda CTN akasema yupo tayari kufanya kazi bure alipewa kazi ya kubadilisha tape.

Alifanya kwa muda na kuona tangazo la chuo cha uandishi wa habari TCJ na kujiunga hapo kwa masomo aliporudi CTN na kuhamia eneo la chumba cha habari kama mwandishi. Na hakuanza kutangaza kama mwandishi na hapo alihamia redio Tanzania.

Aliwahi kumwambia mama yake kwamba atamsikia akitangaza, baadaye akamwambia utaniona  kwenye TV baadaye  tena alimwambia utanisikia  BBC na alikwenda. Anasema uzuri ni kwamba ukijiwekea malengo na unapoyafikia na kuona haijatosha inakupa hamasa ya kufanyakwa bidii na kujua mambo mengi zaidi.

Anasema ukifanya kazi nje unapata faida ya kujua habari nyingi za nje hasa hasa Africa kwa sababu BBC dunia wakija lazima wamuulize kuhusu habari za nchi yeyote hapa Duniani. Pia anasema wameunganisha BBC swahili na michuzi ili kuweza kufanya kuwafikia watu zaidi kwa sababu Michuzi ina washabiki wengi.

2 Comments

 1. Mussa Rashid Ruhamba

  October 15, 2017 at 11:11 pm

  duuuuh the interested story that’s good never give up

  • Roman Olomy

   October 17, 2017 at 4:52 pm

   endelea kufuatilia historia nyingi za watu maarufu ndani ya hii blog

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *