Uncategorized

NI MSOMI, MSEMAJI WA WASANII BONGO SOMA HARAKATI ZAKE HAPA

on

NI MSOMI, MSANII NA MSEMAJI WA WASANII TANZANIA  AMBAYE ANATAMBA NA NGOMA YAKE YA BABA SWALEHE,KIUJAMAA, NJE YA BOX N.K, ANAONEKANA KUWA MJASIRI SANA PALE AMBAPO ALITOA NGOMA YA SITAKI KAZI ILIMFANYA AITWE NA MH. JAKAYA IKULU.

Amezaliwa Arusha mtaa unaitwa Sinoni Daraja Mbili. Katika familia yao yeye ni mtoto wa pili Joh makini wa kwanza akifuatiwa na wodogo zake wawili wa kike. Anawadogo zake wengine watatu wa mke mwingine wa baba yake.

Amesoma shule ya Primary Daraja mbili na huko alikuwa anapenda kucheza mpira sana na pia alipoingia Secondary aliacha kucheza mpira na kuanza kurap. 

Baada ya kumaliza la saba Nikk wa pili alitafutiwa biashara ya kuuza mtumba katika soko la Kilombero, hii ni kutokana na hakuweza kufaulu mwanzoni ila pale ambapo Second selection ilitoka Nikk wa pili alichaguliwa kujiunga na Shule ya secondary Arusha Sec.

Alipoingia shuleni mwenzi wa 5 badala ya mwenzi wa 3 hii ni kwa sababu za uchumi wa nyumbani na kushika nafasi ya pili kutoka mwisho hii ni kwasababu ya kutokujua na kuelewa cha kufanya na kusoma na masomo mengi alikuwa hayajui. Ila baada ya hapo hajawahi kutoka ndani ya tano bora.

kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne alilipa ada mara moja tu. Anasema kwamba baada ya kusoma na kumaliza chuo kikuu ndio alirudi na kulipa ada ili achukue vyeti vyake. Akiwa na rafiki yake Aggrey walitengeneza risiti feki ili kufanya mtiani lakini walikamatwa na kutolewa  nje.

Walipangisha gheto lake na rafiki yake Benja na Aggrey na kukaa hapo katika kipindi chote cha masomo ya O-Leval na walifaulu wote. 

Baada ya kumaliza Form 4 alifaulu na kupangiwa KIGOMA sekondari katika safari yake alilala kwenye basi ndio akaandelea na safari. Alichaguliwa katika kombi ya HGL na KIGOMA SEKONDARI haikuwa kupeleka mwanafunzi chuokikuu. Katika darasa lao ndio waliweza kufaulisha wanafunzi wengi kwenda chuo kikuu.

Baada ya form six alipangiwa CHUO CHA MLIMANI NA KUSOMA sociology pamoja na Public policy. Alianza kurap toka kidato cha kwanza ila hakupenda kuishi kama msanii.

Niaje Niipi alirekodi kama freestyle pale ambapo Joh makini alimuomba amsindikize studio Kama Kawa na kufanya hiyo nyimbo.

Amewahi kufanya kazi NGO’S moja kama Field Officer kwa muda wa mwaka mmja. Ndoto yake yake ilibadilika akiwa sekondari na kutaka kuwa mwanamuziki wa rap hapo mwazo alikuwa anandoto ya kucheza mpira.

Baba yao alipowaona wanafanya muziki hakuwakataza lakini alihofia hadi kumwambia Rafiki yake joh makini. Anasema shule ni kwenda kutafuta maarifa na siyo kwenda kupata nafasi ya kupata kazi baada ya kumaliza. 

Wazazi wanataka kwamba watoto wasome vitu ambavyo watapata kazi na hivyo wanafunzi kukosa muda wa kutafuta maarifa mengine ya kimaisha. Mwanafunzi kubaki kucheza gemu na kuangalia muziki huku wakikariri ili mwisho wa siku wapate kazi. Anasema asilimia kubwa ya elimu ya bongo ni kukariri tuu.

Anasema Joh Makini alichangiwa hela ya kwenda Dar kurekodi na kufikia hapo alipo. Hii ni sababu ya studio kuwa chache na pia alikuwa hajui hatma ya siku yake na hiyo ilimfanya NIKK aamini kwamba KILA KITU KINAWEZEKANA.

Kwa sasa anasoma PHD kwa muda wa miaka mitatu kwa kuhakikisha kwamba anatengeneza proposal yake. Anasema anapenda kuwa mwanasiasa lakini mpaka aone pale ambapo siasa imekuwa kama yeye anavyotaka.

Kwa mawazo yake anaona kwamba uwekezaji umebeba ajira nyingi sana bongo na kuwaacha wananchi hasahasa vijana wakibaki bila kitu.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *