Uncategorized

HISTORIA YA MWANADADA LADY JAY DEE

on

Ni mjasiriamali anamiki Lodge yake inayoitwa NYUMBANI LODGE pia anabendi yake initwa MACHOZI BAND. ni mwanamuziki ambaye anaonekana kuwa na mvuto mkubwa kwa wasichana ambao wanataka kufanya muziki kama kazi. huwa anajihusisha sana na mambo ya kijamii kama kulea yatima.

Judith Wambura alizaliwa mkoani Shinyanga mnamo tarehe 15 Juni,1979 kwa Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujiingiza kwenye masuala ya muziki hapo mnamo miaka ya 2000.

Alianza kujibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la “Machozi” na kutoa single kadhaa kutoka katika albamu hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika bongo flava kwa kutumia gharama kubwa ya ujenzi wa albamu katika historia ya muziki wa kizazi kipya.
Lady Jay Dee ni msanii mwenye kumiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia. Studio inakwenda kwa jina la Jag Records.
Jay Dee, alishawahi kuchaguliwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Kike wa Tanzania kwa muziki wa R&B mnamo 2002, na kutumbuiza katika Kora All Africa Designers Competition, na kutuzwa “Albamu Bora ya R&B” katika Tuzo za Muziki Tanzania kunako tar. 6/8/2004. Kunako mwezi wa Julai 2005, ameshinda tuzo ya “video bora ya msanii wa kike kwa Africa Kusini.

amechaguliwa kuwa balozi wa haya makampuni

 • Mwaka 2009 alichaguliwa kuwa balozi wa  Airtel Tanzania
 • Mwaka 2010 alichaguliwa kama balozi katika Comprehensive Community Based Rehabilitation In Tanzania (CCBRT HOSPITAL)  
 • Mwaka 2012 alichaguliwa kuwa balozi wa NMB ( National Microfinance Bank) Tanzania katika project yao ya “PESA FASTA”
 • Mwaka 2014 alisaini kuwa balozi wa kifataifa wa kampuni ya vipodozi ya Oriflame ya Sweden.
 • Mwaka 2014 alichaguliwa na  Marie Stopes Tanzania kuwa balozi wa uzazi wz mpango Tanzania
 • Mwaka 2015 alisaini kuwa balozi wa Tanzania katika project yao ya HIV/AIDS Geita Gold Mine

tuzo

alizoshinda:
 • 2010 SFC awards – Best Female Artist
 • 2010 – Pearl Music Awards – Best Female Artist from Tanzania
 • 2011 Fiesta Hall of Fame Award
 • 2011 Pearl Music Award – Best Female Artist from Tanzania
 • 2011 Uganda Divas Awards – Best Female Artist from Tanzania
 • 2012 – Baab Kubwa Magazine Awards – Best Female Artist in Tanzania
 • 2014- Tanzania Music Awards – Best Zouk/ Rhumba Song (” Yahaya”)
 • 2014 – Tanzania Peoples Choice Awards – Favourite Female Music Video (“Yahaya”)
 • 2015 Kenya Bingwa Music Awards – East African Song of the Year (“Yahaya “)
 • 2015 Tanzania People’s Choice Awards – Favourite Female Artist
alizoshiriki lakini hakushinda:
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *