LifeStyle

Zijue pia Zitambue Ngazi saba za mafanikio yako katika maisha

on

Mafanikio ni kiu ambacho kila mtu huku duniani hukuhitaji, mafanikio huleta  furaha kubwa katika maisha ya binadamu sasa jua kwamba kuna watu wengi wanapamban a kujua au kufikia mafanikio yao katika ndoto zao ila wanashindwa kuzijua au kuzifuata ngazi ambazo zitaweza kuwafikisha katika kilele cha mafanikio yao ya kuifanikisha furaha katika mioyo yao zitambue ngazi hizo hapa.

  1. Ni nini kwa nini yako?

Watu wengi hufanya mambo ya hapa na pale ambayo husaidia kutimiza ndoto zao ila sasa je ushawahi kujiuliza ni sababu zipi zinazokufanya wewe kufanya unachokifanya lazima ujiulize kwamba nini faida ya unachokifanya je kinakupeleka sehemu chanya au hasi? jiulize .  Jiulize pia unafanya hicho kitu kwa sababu unakipenda chenyewe au unapenda matokeo yake? jiulize ukiweza kupata majibu ya haya hiyo ndiyo ngazi ya kwanza ya kufikia lengo lako.

2. Jua unachokitaka

Usifanye vitu kwa kuwa wengine wanafanya pia usifanye kitu kwa kuwa umejiaminisha kwamba umekosa cha kufanya cha zaidi hakikisha unafanya kitu ukijua kwamba kitakupa kitu ambacho unakihitaji katika maisha yako. Ndugu yangu muda ni sasa muda ndio huu peleka nguvu zako kwenye nyenzo ambazo zitakupa unachokihitaji uzuri wa kufanya hivi ni kwamba moyo wako hufarijika pale unapofanya kitu kitakachokupa mahitaji ya ndoto zako.

3. Penda kufanikiwa kama unavyopenda kupumua

Hapa tafsiri yake ni kwamba hakikisha unaweka nguvu zako zote katika kutafuta na kufikia ndoto zako pia hakikisha unatumia muda wako binafsi kwa kuuwekeza katika kufikia ndoto zako, Pia lazima ndugu yangu upende malengo yako wewe na uyajali kama unavyopenda uhai wako wewe ukiweza kujali ndoto zako kwa namna hiyo basi umefanikiwa.

4. Usijipe sababu

Pale ambapo unakwama katika jambo usijifariji au usijitafutie vijisababu vya  kushindwa tafuta sababu ambazo zitaweza kukupa suluhisho usijifariji kwa kundwa wala usijilaumu kwa kushindwa jipange baada ya kushindwa. Mafanikio ni kutokufanikiwa na kutokufanikiwa ndio mafanikio kwa hiyo la msingi ndugu yangu ni kujisasahihisha pale ambapo unaanguka na siyo kujifariji.

5. Kuwa na mipaka

Usipende kila kitu chako kiwe wazi jiwekee mipaka katika kazi yako, muda wako, maisha yako na marafiki zako hakikisha unaamka pamoja na ratiba yako na pale mtu anakuambia ufanye kitu gafla kataa angalia ratiba yako kama hakuna muda wa kuweza kufanya kitu hicho kitu basi mwambie ukweli zingatia sana kutokufanya vitu ambavyo vipo kinyume na malengo yako.Hasahasa pale ambapo marafiki wanakushawishi ufanye mambo ambayo yako ndani ya malengo yako na siyo malengo yako cha msingi apo ni kujiweka  pembeni na fikra zao na kufuata fikra zako.

Mpaka hapo hizi ndizo ngazi tano ambazo zitakufikisha katika malengo, ndoto na mafanikio yako tafadhali endelea kukaa katika site hii ili uzidi kujifunza mengi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *