Cellebs

HISTORIA YA DIAMOND PLATNAMZ

on

 

Nassib Abdul Juma amelizaliwa tarehe 2 mwenzi wa 1989  ni mtunzi,  mwanamuziki pia ni mfanyabiashara   . Diamond anawatoto wawili Tiffah na Riaz ambao amezaa pamoja na mpenzi wake Zari the boss lady pamja  Msanii huyu anafaamika na kibao ambacho kilimpa umaarufu sana nacho ni “MY NUMBER ONE’ Diamond ameshinda tuza za channel O pia ametumbuiza katika mashindani ya big brother.

Kwa mujibu wa Diamond, mwaka 2008 na 2009 alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8, huku nauli ikimgharimu shilingi 1,000 mpaka kufika kwao na hapo chakula ni zaidi ya shilingi 1,000. “Ukimuona mtu ana mafanikio kiukweli ujue amehangaika sana, mimi katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama ningelikuja kupanda ndege kwa kutumia pesa yangu, namshukuru sana Mungu na haya ni matunda ya kazi ngumu ambazo huwa nazifanya,” alisema. Msanii huyo aliwataka wapenzi wa kazi zake kufanya kazi kwa bidii kwa kipindi kifupi ili kufanikiwa katika maisha yao na kuonekana watu katika jamii na sio kudharaulika.

Diamond anaonekana ni mhamasishaji na mpendwaji mkubwa kwa mashabiki wa muziki wa bongo fleva. Zaidi ya hapo inasemakana ni msanii anayeongoza kwa mapato ya muziki katika nchi ya Tanzania kwa sasa. Pia yeye ndiye msanii ambaye inasemekana anaongoza kwa mauzo ya ringtones katika muziki wa Bongo fleva mwaka 2013 pia ndiye msanii ambaye analipwa ghali katika show zake kiasi cha milioni 100 alilipwa  katika Tigo kiboko yao concert.

Diamond mpaka sasa ametoa ngoma zinazojulikana zaidi ya 30 ambazo ni

 • isachi”
 • pi Sijasikia”
 • “Kamwambie”
 • “Nalia na mengi”
 • “Mbagala”
 • “Nitarejea”
 • “Binadamu”
 • “Kizaizai”
 • “Lala Salama”
 • “Moyo Wangu”
 • “Mawazo”
 • “Kipofu”
 • “Kisa”
 • ″Nimpende nani″
 • “Chanda Chema”
 • “Ukimwona”
 • “Nkifa Kesho”
 • “Nataka Kulewa”
 • “Kesho”
 • “Mapenzi Basi”
 • “Uswazi take away remix”
 • “Nieleze”
 • “Natamani”
 • “Number One”
 • “Number One Remix” (featuring Davido)
 • “Mdogo mdogo”
 • “Bum Bum” (featuring Iyanya)
 • Lala Ukisinzia,Ntampata, Wapi,Nasema Nawe”,Nakupenda pia Nana.
 • Utanipendaga
 • Salome
 • Marry you
 

Diamond ameshinda tuzo 22 katika ya 28 alizoshiriki.

Msanii maarufu kama Simba ni balozi wa makampuni kama vodacom, Cocacola pia watoto wake wameweza kupata kuwa mabalozi mfano Tiffah ambaye ni mtoto wake wa kwanza wa kike ni balozi katika Nmb junior account,Pugu shopping na Msasani shopping mol kwa upande wa nguo za watoto.

Mwaka 2016 alifanikiwa kuwasaini wasanii watatu katika Lebal yake ya muziki inayoitwa Wasafi Classic Baby ambao ni Harmonize, Rich Mavoko na Rayvanny ambao wanafanya vizuri sana pia ameweza kuanzisha mtandao wake wa kuuza muziki wa wasanii mbalimbali inayoitwa Wasafi.com.

 
Diamond amejenga misikiti maeneo mbalimbali Tanzania ikiwemo mkoa wa Morogoro, pia amewajengea watu mbalimbali nyumba katika mkoa wa Iringa kwa ujumla Diamond hupenda kuwasaidia sana wanajamii wenzake pindi anapoguswa na jambo fulani linalohusu jamii.
Mwaka 2017 Diamond amefanikiwa kuzindua bidhaa zake mbili ambazo Chibu Purfume pamoja na Diamond Karanga ambazo zinapatikana Afrika mashariki

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *