LifeStyle

(muhimu soma)Tabia 5 ambazo ukiwa nazo kama mjasiriamali utafanikiwa kwa unachofanya.

on

1. Kuwa na uhuru

hapa nazungumzia uwe huru kifamilia, marafiki ndugu na kubwa zaidi ni mapinduzi ya kifikra amini katika mawazo yako. Pale ambapo unafanya kitu afu unaona unashindwa usikimbie kutafuta mtu mzoefu wa kukusaidia hii itakujengejea kutokuwa na fikra mpya na kuishi kwa kusaidiwa fanya kila namna ili uweze kutatua ilo jambo ndio ukishindwa utafuta mtu wa kukusaidia.

2. Kuwa uwezo wa kujadiliana( negotiation)

Hii itakusaidia wewe kuweza kufanya mauzo au manunuzi ya bidhaa katika kampuni ya kwa upende wa faida zaidi bila kumuumiza mteja au kujiumiza mwenyewe pale unapoagiza bidhaa zako. Kitu ambacho unatakiwa uwe nacho ili kuwa na huu uwezo ni kujiamini mwenyewe na kuamini kazi yako ukifanya makubaliano mazuri na mteja ndivyo unaongeza mapenzi mazuri kwa wateja wako hatimaye kampuni yako itasonga mbele.

3. Fikiria nje ya boksi au tuseme nje ya sanduku.

usipende kufanya vitu kama wengine wanavyofanya jitahidi sana kufanya bidhaa zako kuwa na ubora na mwonekano tofauti na wengine kwa nini bidhaa ziwe tofauti na za wengine? sababu ni moja tuu kinachokutambulisha na kukuza katika soko la kitu unachokifanya na kuifanya kampuni yako ijulikane zaidi na kupenda ni ule utofauti wako wa ubora, mwonekano na uimara wa bidhaa yako mbele za macho ya watu.

kama ulizoea kuchukua mzigo sehemu fulani ebu nenda tena sehemu nyingine kuchukua hii itakufanya uwe na uelewa wa soko katika maeneo mbalimbali.

4. Jifunze kutokuwa na matumizi yasiyo ya lazima

hii kwa wale wanapenda kuangalia au kutumia kila kitu ambacho siyo lengo katika biashara zao au maisha yao mfano kuangalia vitu ambavyo havina maana katika mtandao kama vile picha za ngono, vichekesho au nyimbona kwa muda mrefu hii hukupotezea muda wako pamoja na na kipato chako mjasiriamali lazima uwe bahili epuka michango ambayo si ya lazia epuka sherehe ambazo si za lazima fanya mambo kwa ratiba na fuatilia zatiba yako.

5. Punguza matumizi ya kawaida

kujinyima ni hatua makini ambayo ukiitumia vizuri unaweza kutima ndoto zako za kijasiriamali.. mfano huna familia kubwa na unaamua kupanga nyumba kubwa ya kuishi na kulipa kodi kama laki mbili kwa mwenzi huku unandoto ya kuwa na pikipiki yako za kubeba abiria baada ya mwaka mmja. hapo ni bora ungepanga nyumba ya elfu hamsini alafu laki na hamsini uweke kwenye kibubu baada ya mwaka utakuwa na milioni moja na laki nane  ambayo utaweza nunua pikipiki bila hata kukopa.

punguza kunywa vitu kama pombe,soda, manunuzi ya nguo n.k baadaye ya mda utaona matokeo chanya katika biashara yako.

document.write(“”);Kaa karibu na blog hii ili kuweza kupata makala mbalimbali za kiafya, kimaisha na kijasiriamali ambazo zimeandaliwa na kijana mpenda maendeleo Romani a.k.a NJIBA karibuni sana sana sana

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *