Uncategorized

BIASHARA AMBAZO UNZWEZA FANYA UKIWA NA MTAJI MDOGO

on

Mitaji imekuwa kikwazo kikubwa katika kuanza biashara nyingi sana. Sababu nyingine ni kuwa watu wengi wanaofikiria kuanza biashara wanataka kuanza na mitaji mikubwa kama milioni 5 -10 au zaidi. Ukweli ni kwamba hiyo ni ngumu hasa kwa nchi ambazo ni maskini kama Tanzania.
Mwishowe mawazo mengi ya biashara yanakufa kabla ya kuanza.Wataalamu wa bishara wanaeleza kuwa kuanza ni kugumu na ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya wajasiliamali wengi.Ukweli ni kuwa kuna biashara nyingi tu ambazo hazihitaji mitaji mikubwa kuanza.
1. KufundishaTafuta kitu ambacho unakifahamu na angalia jinsi utawapa watu elimu yakoMfano unaweza ukawa ni mtaalamu wa kupika keki tamu. Basi unaweza ukaanda darasa la watu katika maeneo unayoishi na kuandaa mafunzo kwa ada ndogo nyumbani kwako.Unahitaji kiasi kidogo tu cha fedha ili kutimiza hilo.Pia unaweza ukafundisha watoto masomo ya ziada kama hesabu au sayansi kama unaufahamu wa masomo hayo au mengineyo.Vyote hivi havihitaji hela nyingi kuanza kwasababu huhitaji chumba cha biashara wala fanicha.
2. Biashara ya Mtandao

Jiunge na kampuni inayofanya masoko kwa njia ya mtandao. Makampuni haya yatakuhitaji wewe kuafanya matangazo kwa njia ya mdomo kwa mtu hadi mtu kwa kuwaeleza juu ya bidhaa za kampuni husika na wakinunua basi kampuni itakulipa wewe kiasi cha fedha kwa mauzo yaliyofanyika.Usajili katika biashara hii kunahitaji mtaji mdogo sana hata kwa Sh. 100,000 tu unaweza ukaanza na kuendelea kukuza mtaji.

3. Kutoa Ushauri wa Kitaalamu


Kama wewe ni mtaalamu katika nyanja fulani kama vile fedha,afya au komputa kwa mfano,unaweza ukaanzisha huduma ya ushauri kwa makampuni madogo au watu binafsi.Ili kufanya hivyo utahitaji fedha kidogo tu kwaajili ya vitendea kazi kama vile karatasi, kalamu n.kUtahitaji kujitangaza kwa kupita ofisi hadi ofisi au kwa kutoa matangzao katika radio ,TV au magazeti.Unaweza kutumia ofisi za wateja kwajili ya kazi hii hivyo kuwa na ofisi. Tumia sehemu unayoishi kama ofisi hivyo ngarama itakuwa ndogo sana.
4. Huduma ya Kutunza Watoto Wadogo

Kutunza watoto wadogo kati ya mwaka 1-5 ni biasahara ambayo unaweza ukaianzisha na kuifanya nyumbani na itahitajifedha kidogo tu.Wazazi wenye watoto wanahitaji sehemu ambayo watoto wao watapata huduma wao wakiwa kaziniKama ukianda mazingira mazuri ampapo watoto wanaweza kucheza na kujifunza,basi utapata wateja wengi.
5. Kuwa na kipundi  cha kupika

hii ni kazi ambayo kwa sasa inafanya vizuri sana kwa sasa kwa sababu sherehe kwa sasa zipo nyingi karne ya sasa watu wanafanya sherene za ubatizo,kipaimara,komunyo, siku za kuzaliwa na maharusi kwa hiyo ukiweza kuwa na kikundi ambacho kipo vizuri sana. mtaji wake siyo mkubwa kikubwa ni gharama.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *