Cellebs

Mfahamu Roman Reigns

on

Leati Joseph Anoa’i amezaliwa 25/5/1985 huko Pansacola Florida Marekani ni mwanamieleka ambaye ni maarufu kwa jina la Roman Reings sana pia baba na mama yake wote walikuwa wacheza mieleka yeye ni binamu wa kina Umaga, Yokozuna,Rikishi na the Tonga Kid Reings amemuoa mwanamama Galina Joelle mwaka 2014 na kupata nae mtoto mmja wa kike.

Amecheza mpira wa miguu akiwa katika Pensacola Catholic high school kwa muda wa miaka 3 , kisha alihamia katika shule ya Escambia kwa muda wa mwaka mmja. Alifanikiwa kutajwa kama beki bora katika jarida la  Pensacola news journal,  Alifanikiwa kujiunga katika chuo kikuu cha Georgia Institute of Technology na kufanikiwa kuanza katika kikosi cha All-Atlantic Coast Conference mwaka 2006 baada ya kuwa na rekodi rudi ya kuzuia katika nafasi yake kama beki. baada ya kucheza ligi kuu ya Marekani alisajiliwa na timu kama Minnesota Vikings, Jacksonnivile Jaguars , Edmonton na Hilmiton Tiger cats. Mbili za mwisho zilikuwa zikicheza katika ligi kuu ya Canada.

Mwenzi wa saba 2010 aliingia rasmi katika michezo ya mieleka katika kampuni ya World Wresling Entertainment na kuanza kucheza katika Florida Championship Wresling akiwa akijulikana kama Roman Leakaee aliendelea kupambana hapo na mwaka 2011 alifanikiwa kushinda Taji la Hevyweght Championship baada ya kumpiga Krugger kisha baadaye kushinda katika triple threat Match dhidi ya Dan Ambrosse na Seth Rollins ila alishindwa kutetea taji hilo baada ya kupigwa tena na Krugger na kupokonywa mkanda huo. mwaka 2014 alifanikiwa kushinda tuzo ya superstar bora wa mwaka “Slammy Award”

Mwenzi wa kumi 2016 alifaniiwa kuwapiga Alberto Del Rio, Dolp Ziggler na Kelvin Owens kisha kushinda Hevyweght Championship mwenzi wa nne 2016 alifanikiwa kumpiga Triple  H na kushinda mkanda wa WWE World Hevyweght Championship, Roman Reigns alifanikiwa kupiga Rusev katika mechi ya ubingwa wa United Championship katika hell in the Cell na kufanikiwa kuchukuwa ubingwa huo , kwa sasa amefanikiwa kumpiga undertaker mara mbili hivyo kuzidi kuonyesha ubabe katika michezo hiyo.

 

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *