Health&Food

Yafahamu magonjwa au maradhi ambayo huambukizwa hosipitalini.

on

Haya ni maradhi ambayo huambukwa baada ya kukaa maeneo ya hosipitali kwa muda wa masaa 24, maradhi haya huweza kumwadhiri hata mgonjwa ambaye amelazwa wodini, Tatizo hili lipodunia nzima na kwa nchi ya Tanzania asilimia kumi ya wagonjwa ambao wanalazwa hospitalini hupata maradhi haya. Yafuatayo ndio maradhi ambayo mtu, ndugu au mgonjwa hupata akiwa hospitalini;-

 • Maradhi ya mtoto mchanga na mama mjamzito au mama aliyejifungua.
 • Maradhi unayoyapata baada ya kufanyiwa upasuaji
 • Kuharisha
 • Nemonia
 • U.T.I
 • Maradhi unaweza kupata baada ya kuwekewa sindano mkononi,mpira wa mkojo na mpira wa kumlisha mgonjwa.

Visababishi vya maradhi haya ni kama vifuatavyo;-

 • Muuguzi au daktari kumuhudumia mgonjwa kwa kutumia vifaa ambavyo siyo visafi.
 • Hewa ;- wagonjwa wenye maradhi ya kifua kikuu kuchanganywa na wengine,
 • Ndugu wanaotunza wagonjwa kuwahudumia wagonjwa bila kutumia vifaa vya kujikinga.
 • Wauguzi au madaktari kuwahudumia wagonjwa  bila kutupima vifaa vya kujikinga.
 • Wagonjwa kushirikiana au kupeana vifaa vya kutumia.

Makundi ambayo yapo katika hatari ya kupata maradhi haya;-

 • Wauguzi
 • Madaktari
 • Wafanyakazi wengine walioo ndani ya hosipitali
 • Wagonjwa wanaokaa muda mrefu hosipitali
 • Ndugu, jamaa na marafiki wanaotunza wagonjwa wodini au wanaokuja kuwasalimia wagonjwa.
Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *