Cellebs

Mfahamu msanii mwanadada Nandy

on

Faustina Charles maarufu kama Nandy ni msanii, mwandishi wa muziki na mwanamitendo wa nguo za kiasili kutoka nchi ya Tanzania, kipaji chake kilianza kuonekana kwa mtayarishaji wa miziki anayeitwa Akili the Brain akiwa chini ya studio hiyo alibahatika kurekodi nyimbo nne lakini hazikufanikiwa kupigwa katika radio stations.

Baada ya kusikia kuna mashindano ya uimbaji katika nchi ya Nigeria lilikuwa linaitwa Kareoke mnamo mwaka 2016 na kufanikiwa kuwa mshindi wa pili na kushinda kiasi cha milioni 36 za kitanzania. Kampuni ya kusimamia mziki inayoitwa Chocolate city iliyopo Nigeria ilitaka kumpa kandarasi mwanadada huyu lakini alikataa na kusema ataenda kujiusisha na maswala ya muziki nchini Tanzania.

Baada ya kuja Tanzania Nandy alianza kujihusisha na maswala ya mitindo yanguo na kuanzisha kampuni yake inayoitwa Nandy African Print na kufanikiwa kuwavisha watu maarufu kama Tulia Atison ambaye ni naibu Spika wa bunge la Tanzania, Pia alijiunga na Tanzania House of Talent (THT) na kufanikiwa kutoa kibao chake cha kwanza kinachoitwa Nagusagusa na baada ya hapo alitoa nyimbo kama wasikudanganye, one day, Mahabuba akiwa ameshirikiana na Aslay zote zikiwa zimefanya vizuri katika chati mbalimbali nchini na Afrika kwa ujumla.

Mwaka 2017 alifanikiwa kushinda Tuzo ya mwanamuziki bora wa kike Afrika Mashariki katika tuzo za AFRIMA.

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *