Cellebs

Mfahamu kiundani zaidi Zinedine Zidane “Zizou”

on

Zinedine Yazid Zidane amezaliwa tarehe 23 mwenzi wa sita mwaka 1972 katika mji wa Marseille huko Ufaransa, kiasili zidane anaasili ya Algeria Baba yake na mama yake walikimbilia Ufaransa kabla ya kuanza vita huko Aligeria mwaka 1953. baba yake alikuwa akifanya kazi ya ulinzi na mama alikuwa akifanya kazi za nyumbani tuu. Mwaka 1994 alifanikiwa kufunga ndoa na mwanadada Veronika wakafanikiwa kupata watoto wanne wote wa kiume

 

Akiwa na miaka mitano Zidane alianza kucheza Mpira katika kiwanja cha ukubwa wa upana wa mita 12 kwa urefu wa mita 80 katika eneo linaloitwa Castellane , baada ya kufikisha miaka 10 Zizou alipata nafasi ya kupewa leseni na kusajiliwa rasmi katika timu ya US Saint Henri ya watoto ya klabu ya Castellane alikaa kwa muda wa mwaka mmja na nusu kisha akahamia katika timu ya SO Septemes baada ya kocha wa timu hiyo anayeitwa Robert Contenero kulazimisha uongozi umchukue Zidane. Alipofikisha miaka 14 zidane alipata nafasi ya kwenda kufanya mazoezi ya viungo na kucheza mpira wa miguu katika kituo kinachoitwa Aix En Provence kinachomilikiwa na Shirikisho la mpira la Ufaransa, hapo alionekana na kuchukuliwa na klabu ya AS Cannes.

Alifanikiwa kujiunga na AS Cannes kwa mkataba wa miaka 4 bosi wa timu hiyo alimchukua na kuishi naye nyumbani kwake, Akiwa klabuni hapo Zizou alishauriwa kupunguza hasira kwani alikuwa akiwaiga ngumi sana wenzie na kupelekea kuewa adhabu ya kufagia katika eneo la klabu mara kwa mara. Mwaka 1989 mwenzi wa Tano alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Nantes katika ligi  Ufaransa kisha 1991 mwenzi wa kumi alifunga goli lake lla kwanza kama mchezaji wa kulipwa dhidi ya Nantes na kupewa zawadi ya gari na mwenyekiti wa timu yake ya AS Cannes.

Mwaka 1992 alijunga na timu ya Bordeaux kisha kushinda kikombe cha Intertoto cup pia akawa mchezaji bora wa ligi ya ufaransa mwaka 1996. Alijiunga na Juventus mwaka 1996 kisha akafanikiwa kushinda klabu bingwa Italia pia kushinda kikombe cha klabu bingwa dunia mwaka 1996 pia alifanikiwa kuwa mchezaji bora wa dunia mwaka 1998 kisha mchezaji bora kwa wachezaji wanaotoka nje ya Italia mwaka 2001.

(Pichani ni Zinedine Zidane akiwa na mke na watoto wake nne pamoja na mwenyekiti wa klabu ya Real Madrid )

mwaka 2001 zizou alijiunga na Real Madrid kwa ada ya Euro Milioni 77.5 na kuweka rekodi duniani ya kuwa mchezaji ghali zaidi, 2002,03 alifanikiwa kuchukua ubingwa wa la liga, 2003 alifanikiwa kuwa tena mchezaji bora wa dunia kisha 2004 mashabiki walimchagua kama mchezaji bora wa ulaya kwa miaka 50 iliyopita, kisha mwaka 2006 alitangaza rasmi kustaafu kucheza mpira wa miguu.

Alianzia kucheza timu ya Taifa mwaka 1994 katika mechi dhidi ya Cshek Repablican kisha mwaka 1996 alifanikiwa kucheza kombe la dunia kisha Ufaransa ikatolewa katika hatua ya Nusu fainali, Mwaka 1998 katika kombe la dunia zidane alicheza vizuri sana pamoja ba timu yake ya taifa ya Ufaransa na kufanikiwa kufunga goli 3 dhidi ya 0 walizopata Brazil huku yeye akifunga Magoli 2 kisha wakachukua Kombe la Dunia.

mwaka 2000 Akiiongoza Ufaransa walifanikiwa kushinda kombe la Euro na kuwa nchi ya kwanza kuweza kushinda kombe la dunia na kombe la Ulaya. 2002 alicheza kombe la dunia lakini Ufaransa walitoka katika hatua ya makundi, 2006 walicheza kombe la Dunia na kufika hadi hatua ya fainalli ambapo Zidane alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa beki wa Italia Marko Materazi.

Mwaka 2016 Real Madrid walimtangaza rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo na mpaka sasa amefanikiwa kuwapa ubingwa wa klabu Bingwa ulaya na Ubingwa wa klabu bingwa dunia.

Amechukuwa vikombe tofauti tofauti 13 akiwa kama mchezaji na ameweka rekodi tisa tofauti tofauti katika maisha ya uchezaji wake wa mpira amekuwa mchezaji bora mara 45 katika mashindano tofauti tofauti. Zidane ameweka rekodi baada ya kuisimamia timu ya Real Madrid ya kuweza kuchukua kombe la ligi ya klabu bingwa ulaya mara mbili mfulilizo 2016 na 2017 pia ameweza kuchugua ubingwa wa ligi kuu ya Hispania La Liga mwaka 2017

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *