Cellebs

Mfahamu kiundani zaidi msanii Aslay

on

Isihaka Nassoro amezaliwa tarehe 6 mwenzi wa tano mwaka 1995 katika mkoa wa Dar es salam na kupata elimu yake ya msingi katika shule msingi Yusuph Makamba kati ya mwaka 2003 hadi 2009 kisha akajiunga na masomo ya sekondari mwaka 2010 na kumaliza kidato chake cha nne mwaka 2014. Mwaka 2015 aliondokewa na mama yeke kipenzi pia mwaka huo huo aliweza kupata mtoto wake wa kwanza na kuanza kujiita “dingi mtoto”

Kaka yake anayeitwa Idd ndiye aliyegundua kipaji chake akamchukua na kumpeleka kwa Mdau wa muziki hapa Tanzania Said Fella anamiliki TMK, Fella akishirikiana na Chambusso walimjumuisha Aslay katika kundi la Mkubwa na Wanawe. Mwaka 2011 alishiriki katika Tamasha la majahazi huko Zanzibar na kuimba wimbo wa Zuwena, mwaka huohuo alitoa nyimbo yake ya kwanza inayoitwa “Nitakusemea” ambayo iliwagusa sana watoto na wamama mwaka uliofuata 2012 alitoa nyimbo yake nyingine inayoitwa “Umbea” akiwa amemshirikisha Chege kisha 2013 alitoa nyimbo nyingine inayoitwa “Bado mdogo”.

Mwaka 2013 kwenda 2014 mkubwa Fella aliunda kundi la Yamoto Bend ambalo liliundwa na wasanii Aslay, Maromboso, Beka Flavour na Mbosso, Kundi hilo lilitoa nyimbo mbalimbali kali na kubwa sana mwaka 2017 mwanzoni kundi hili lilivunjika na kumruhusu kila msanii kutafuta meneja wake na kufanya muziki mwenyewe.

Aslay alibaki na meneja wake wa zamani Chambuso na kutoa nyimbo kali mfululizo kama vile Angekuona, Usiitiedoa akiwa na Khadija Kopa, pusha, muhudumu, baby na Natamba sababu ya yeye kutoa nyimbo zaidi ya tano ndani ya mienzi kama miwili ni ili yeye aweze kumudu jukwaa bili kuimba nyimbo za yamoto band.

Msanii Aslay ameweza kununua Gari aina ya BMW mwaka huu ikiwa ni mafanikio ya muziki wake pia amejenga nyumba.

Mtokambali 728x90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *