Cellebs

Mfahamu msanii mkongwe wa Uganda Dr Jose Chameleone kiundani

on

 

 

Joseph Myanja maarufu kwa jina la Dr Jose Chameleone amezaliwa mwaka 1979 katika nchi ya Uganda huko ukanda wa Afrika Mashariki. Amefunga ndoa na mwanadada anayeitwa Daniella Atim na kupata nae watoto wanne Ni msanii mkongwe wa muziki wa miondoko ya Hiphop pia Ragga amejizolea umaarufu mkubwa sana katika bara la Afrika kwa uwezo wake wa kuimba na kutunga nyimbo za kiswahili fasaha pengine kushinda hata wasanii ambao watokea katika maeneo ambayo kiswahili ndiyo lugha rasmi hivyo kukitangaza sana Duniani.mdogo wake ambaye wamewahi kuingia katika ugomvi wa kimuziki, anayetumia jina la kisanii la Weasel , pia ni mwanamuziki.

 

Chameleone alianza kama Dj wa klabu za usiku mwaka 1990 kisha wasifu wake mwishoni mwa miaka ya 1990, watengenezaji wake wa muziki wakiwa Ogopa Djs kutoka kenya. Moja kati ya nyimbo zake ya kwanza ilikuwa “Bageya”, ikimshirikishaRedsan, msanii kutoka Kenya. Pia alishirikiana na mwananchi mwanamuziki mwenzake Bebe Cool, lakini baadaye iliiibuka kuwa wawili hawa walikuwa na upinzani mbaya.
Mtindo wa Chameleone wa muziki ni mchanganyiko wa muziki wa tamaduni wa Kiuganda, rumba ya Kati ya Afrika, Zouk na ragga. Albamu yake ya kwanza ilitolewa nchini Kenya mwaka wa 1999. Tangu wakati huo ametoa albamu kadhaa zikiwa pamoja na “Bageya” mwaka wa 2000, “Mama Mia” mwaka wa 2001, “Njo Karibu” mwaka wa 2002, “The Golden Voice” mwaka wa 2003, “Mambo Bado” mwaka wa 2004 na “Kipepo” mwaka wa 2005. Amewahi kuwa mwanamuziki wa kumi kwa utajiri barani Afrika

Yeye ni mwanachama wa Jamii ya Mwanamuziki, muungano wa wanamuziki ambao hutumia umaarufu wao na mali yao kusaidia kuondoa umaskini na kujenga kampeni za mwamko wa UKIMWI VVU.
Ametembelea idadi ya nchi za ng’ambo zikiwemo Marekani, Uingereza na Sweden na nyingine nyingi mno. miongoni mwa mengine.
Mpaka sasa anaalbamu zaidi ya kumi pia ameshinda tuzo 16     kati ya tuzo 36    alizoshindanishwa 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *