LifeStyle

MAMBO 6 AMBAYO YATAKUFANYA UFANIKIWE PALE UNAPOKWAMA

on

1. Tambua mafanikio hayaji haraka lazima kuchukua  uwe mvumilivu pia mpambanaji.

2. Jua kutengeneza mafanikio huchukua muda mrefu kuliko unavyofikiri kwa mara ya kwanza, kwa hiyo lengo lako usiliweke katika hali ya miaka michache pale unapoona kikwazo ndio kujiuliza muda uliojiwekea unatosha? kama hautoshi lazima uongeze ili kuepusha ukataji tamaa.

3. Tambua kuwa watu wenye mafanikio duniani hupata changamoto nyingi na ugumu mwingi kisha hufanya maamuzi magumu  baada ya hapo huvuna kwa faida nguvu zao walizowekeza kiakili na kimwili.

4. Jua kwamba kushindwa ndio kufundishwa jinsi ya kufikia malengo yako, mafanikio ni matokeo ya maamuzi mazuri na ya busara uliyofanya wakati wa kukumbana na kupambambana na changamoto zako.

5. Weka akili kwamba watu ambao wanakuwa na wewe sambamba katika kipindi cha mafanikio ni wengi sana , pia watu watakao kuwa na wewe katika kipindi ambacho unapambana na matatizo na changamoto za maisha ni wachache sana

6. NI NGUMU KUFANIKIWA HUKU UNAFANYA KITU AMBACHO UNAKICHUKIA, NI BORA KUTUMIA NGUVU ZAKO ZOTE KATIKA MAISHA KWA KUFANYA KITU AMBACHO UNACHOKIPENDA KATIKA MAISHA YAKO KUTOKA MOYONI.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *