Uncategorized

MBINU 13 ZA KUWA JASIRI NA KUFANIKIWA KIMAISHA

on

Mbinu 13 na rahisi za kupata ujasiri ujasiri kimafanikio.
1. Kutoshindana na waliofanikiwa.

Daima mtu ahakikishe anawafanya waliofanikiwa wajione wapo juu. Kama mtu anataka kuwashangaza basi asionyeshe ujuzi wake wote.
Kuwapa waliofanikiwa heshima yao kutamfanya mtu apate msaada na hatimaye afikie kiwango cha juu bila ya kupata tabu nyingi.

Mfano, mtu asishindane na mwajiri wake ili kuonekana anajua sana;
asishindane na tajiri katika matumizi hususani mazingira ya kijamii kama
baa, misiba n.k. Waliofanikiwa hutafsiri kitendo cha kushindana kama
kuonyesha kiburi au maskini jeuri.

2. Kutoamini sana marafiki.

Mtu awe makini ‘anapojamiiana’ na marafiki au watu wa karibu. Watu wa
karibu huwa wasaliti na huvujisha siri kwa wapinzani. Mtu aogope
marafiki zaidi ya maadui, ikibidi awape nafasi wale anaohisi ni
wapinzani. Ilkiwa mtu hana wapinzani, ajitahidi kuwatafuta. Mtu ajifunze
jinsi ya kutumia wapinzani kimafanikio, si kuwaamini marafiki muda
wote.

3. Kuficha malengo.

Mtu afiche matarajio yake au dhamira za matendo yake. Kuweka malengo
hadharani huwafanya watu wenye nia mbaya kujipanga na kuvuruga malengo
husika. Mtu akinge malengo yake na ikiwa yatagundulika iwe nyakati za
mwisho; nyakati ambazo wapinzani hawawezi kuweka vikwazo.

4. Kutumia wasidizi.

Kufankiwa kwa mtu kunategemea mchango anaoupata kutoka kwa wale
wanaomzunguka (mazingira na marafiki). Mtu atumie busara, ujuzi na
maarifa ya wale anaofanya nao kazi ili kusonga mbele. Msaada haupunguzi
tu nguvu, bali pia huongeza ufanisi na kuimarisha urafiki. Mtu hupata
fadhila kutoka kwa wasaidizi wake, ndipo jamii husika. Hivyo, mtu
awaachie watu wengine yale wanayoweza kufanya kwa ufanisi.

5. Kushinda kupitia matendo.

Ushindi mtu anaopata kupitia maneno haufai kitu! Mtu asishindane juu ya
uwezo wake kwa maneno bali, aache matendo yaongee. Ushindi makini ni ule
mtu anaoupata kupitia matendo yake, na si kwa wingi wa maneno. Uhalisia
wa matendo huonyesha umakini wa mtu kwa jamii inayomzunguika. Mtu
husifiwa kwa kadiri ya juhudi zake za hali na mali kutatua changamoto
zinazomsonga, si kwa kupiga domo.

6. Kujenga utegemezi.

Ili mtu kujua umuhimu wake katika jamii anapswa kjua kwa kiasi gani
mchango wake unahitajika. Mtu ajenge mazingira ya kutegemewa; kutegemewa
kuleta furaha au ustawi katika mazingira yanayomzunguka.

Ili kfanya hivyo, mtu asitoe mbinu zote alizo nazo juu ya kitu fulani.
Kutegemewa humwezesha mtu ‘kuuza’ kile alichonacho kwa mafanikio yake na
ya jamii yake. Hivyo, mtu ajue wakatigani wa kuficha huduma yake,
wakati gani wa ktoa kidogo na wakati gani wa kutaka watu wailipie.

7. kutenda kama mpelelezi.

Ni muhimu sana mtu kujua juu ya wapinzani wake. Mtu atumie marafiki
(wapambe) ili kupata taarifa muhimu juu ya udhaifu na uwezo wa wapinzani
wake. Kufanya hivyo kutamwezesha mtu kupanga mipango ya kiulinzi na
ambayo haitazimika katika safari yake ya mafanikio. Kupata taarifa
kunafanikishwa kwa kuuliza maswali rahisi, kuuliza kwa njia ya upole na
kwa kutumia mifano. Kila wakati ni fasaha kwa upelelezi.

8. Kuwafahamu watu wa karibu.

katika mazingira yoyote yale kuna watu wa aina nyingi. Watu hutofautiana
kiimani, kitabia, kimalengo, kiutendaji n.k. Watu wa karibu ndio
wanaotoa au kufanikisha kotoa ushindani katika mazingira yasiyotegemewa.
Watu wengi, tena wa karibu ni kama mbwa mwitu. Ili kufahamu watu wa
karibu, mtu atafakari kwa kina misingi mikuu ya urafiki huku
akibadilisha muonekano, kutoa changamoto kwa walengwa n.k. Pindi mtu
anapofanya yote hayo atazame mwitikio ya walengwa.

9. Kuwa na dira.

Dira humwezesha mtu kufika kule anakotaka. Mtu anapaswa kuweka malengo
juu ya kule anakotaka kufika baada ya muda fulani pia, changamoto
azazohisi zitamkumba sambamba na suluhu sahihi. Kwa kuwa na malengo
haitakuwa ngumu sana kukabiliana na vikwazo mtu awapo safarini. Watu
wengi huweka malengo huku wakisahau au kupuuzia adha zinazoweza
kuwakumba au zilizowakumba watu wengine waliokuwa na malengo kama yao.

10. Kujikuza.

Mtu asipokee na kukubali sifa ‘chafu’ anazopewa na jamii. Mtu anapaswa
kujikuza kwa kuvaa utambulisho mpya; ambao unavuta umakini na hauiudhi
jamii yake. Mtu anapaswa kutawala taswira yale, si taswira yake
ktawaliwa na nguvu kutoka nje. Kujikiza kwa jitihada za mtu huleta
taswira ya kudumu, na ambayo italeta uaminifu wa kweli na kukubalika
katika jamii.

11. kuwa na shabaha.

Mtu anapaswa kuelekeza nguvu na jitihada kwa yale anayoamini yataleta
matunda mazuri. Mtu awe makini kutunza au kutenga nguvu za ziada kwa
ajili ya changamoto. Ili kutokata tamaa, mtu anapswa kuwa na wadu (watu
wa karibu) wenye uwazo tofauti tafauti kama vile madaktari, wafanya
biashara, waalimu, viongozi wa dini, wazee wenye busara n.k

12. Kujirudisha nyuma.

Kama mtu akiona changamoto zitamzidi siku a usoni, huku mbinu alizo nazo
au mikakati yake itakuwa dhaifu ahairishe ‘pambano’. Kurudi nyuma
kutampa mtu nafasi ya kujipanga kwa kukusanya nguvu na ‘kuusoma mchezo
zaidi’. Mtu asikubali kuangushwa kabisa na changamoto ndipo ajiandae
kuinuka. Ni vigumu sana mtu kuamka baada ya kushambuliwa na kuangamizwa
na chahangamoto za kimaisha.

13. Kutojitenga.

Kujitenga na jamii au marafiki ni hatari sana! Kwani ulimwengu ni
tambara bovu na uumejaa wapinzani kila kona. Inapasa mtu kujiundia ngome
ya ulinzi lakini, si kwa kujitenga. Kujitenga hupunguza mawasiliano na
watu na pia uwezekano wa kupata misaada ya hali na mali. Kwa mfano, kuna
uwezekano mkubwa wa kukosa habari, ushauri, vitendea kazi n.k. Vitu
ambavyo ni muhimu kufikia mafanikio.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *