Uncategorized

MANENO YA HAMASA SEHEMU YA KWANZA

on

Kama ukifanya mara moja rudia tena na tena na tenaaaa!!!!!
Hamasa inakufanya uwe na msimamo, nidhama na kufanya kwa bidii unachotaka kufanya. pale ambapo unapata hamasa ya kufanya kitu usichukue hasira kaa chini tulia andika kwa mpangilio unachotaka kufanya alafu soma kila kitu hivyo hamasa ya kufanya kitu itajengeka katika maisha yako. unaweza kutumia hiyo hamasa ili kufanya mambo yako na kufanikiwa.
Muda mwingine unaona mambo yako hayaendi vizuri usikate tamaaa endelea kufanya endelea kufanya, usiache kufanya fanya tena na tena na tenaaaaaaa!!!!!
Kitu ambacho kinafanya maisha yetu yabadilike ni matendo tunayofanya na pale ambapo tunashindwa kufanya tunachokiwaza kuelekea katika matendo sababu kubwa ni uoga kwa hiyo pale ambapo unawaza kitu usiogope kufanya kwa vitendo narudia tena fanya kwa vitendoooooooo.
Lazima tujisukume wenyewe ili kufanya maamuzi kwa sababu mabadiliko siku zote huja kwa mtu anayefanya maamuzi maamuzi hayaji kama kitu hata siku moja, maamuzi huja kama vile njaa inapokushika na chakula huna na kuamua kuingia jikoni ili kukipika maamuzi pia huja hivyo hivyo lazima ukae utafakari na ubongo wako na mwili kukubali kuamua kubadilika.
Lazima ujitengenezee hali ya kuwa na maamuzi sasa utafanyaje? fanya mara ya kwanza pima ukipata tatizo la kukufanya usifaulu tafuta sahihisho alafu fanya tena mara pili hakikisha mara ya pili ulisahihisha changamoto ya kwanza, kama imejitokeza tena fanya mara ya tatu rudia tena na tena na tena mpaka pale unaona kwamba fanikio la kwanza limekuja endelea tena ili kuhakikisha unayafanikisha yote. 
Hata kama unaona kwamba unachokifanya hupati faida kipesa lakini kinakupa faida kiakili na kinakufanya unasaidia watu usiachee kwa sababu unatakiwa kuamini Mungu yupo nawe na chochote unachotaka mungu atakupa.

USIACHE HATA KIDOGO RUDIA TENA NA TENA NA TENA MPAKA UHAKIKISHE UMEFANIKISHA

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *