Uncategorized

MANENO YA HAMASA SEHEMU YA III

on

Najua kwa watu wengi wanashindiwa kuelewa kwa nini hawafanikiwi kwa kile ambacho wanakipanga hata kama hata kama mtu hajaweza kuamua au kuthubutu kukifanya katika matendo au tendo ambalo linaonekana kwa macho ya nyama. Pale ambapo anawaza kitu cha kufanya hapohapo mawazo ya kutoweza kukifanya yanaanza kuja ndani ya fikra zake.

Unachotakiwa kukifanya ni kuwa na imani na uwezo ambayo Mungu amekujalia katika kufanya kitu ambacho umewaza kukifanya katika maisha USIOGOPE kukifanya Njia nzuri ya kuweza kukifanya kionekane ni KUKIWEKA KATIKA MATENDO NA KUKIFANYA KATIKA MATENDO NA FIKRA.

Matendo yatakusaidia kuona mapungufu katika wazo lako na mawazo yatakusaidia kutatua changamoto katika matendo ambayo unafanya ili kufanikisha wazo lako. JIAMINI kwamba wewe unaweza kufanya malengo yako yatimie.

Pia tambua kwamba mafanikio huambatana na kushindwa na ILI UFANIKIWE KATIKA MAISHA UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUFANIKIWA KUPAMBANA NA KUSHINDA CNANGAMOTO, VIKWAZO NA MATATIZO AMBAYO YANAJITOKEZA KATIKA NJIA YA KUFIKIA LENGO LAKO.

Achana na mambo ya KUJIOMBEA MWENYEWE MSAMAHA eti sijafanya kwa makusudi imetokea bahati mbaya kwa hiyo sitarudia tena huo ni UONGO AMBAO UTAKURUDISHA NYUMA. jifunze KUJIADHIBU pale ambapo unaona hujatimiza unachokihitaji mfano kama unajaweza kufanya kitu kwa muda uliopanga ongeza muda wa kufanya punguza muda wa kupumzika.

JIFUNZE KUFANYA KITU KWA ASILIMIA MIA MOJA hii itakufanya wewe upambane kiasi kwamba ufikishe asilimia mia moja na kukufanya wewe kuumia sana pale ambapo unapata chini ya asilimia 50%  kwa hiyo itakufanya wewe kukazana na kuongeza bodii katika mipango yako ya maisha. 

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *