Cellebs

HISTORIA YA RAPPER JAY MO

on

 Juma Mohamed Mchopanga (amezaliwa tar.27 mwenzi wa 11 mwaka 1978) ni rapa wa muziki wa hip hop kutoka nchiniTanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jay Moe. Pia anajulikana kwa vibao vyake mashuhuri kama vile BishooJua na MvuaKama Unataka DemuMaisha ya BodingStori Tatu Tofauti, na Sihitaji aliyofanya na Lord Eyez wa Nako 2 Nako. Jay Moe ni mmoja kati ya waanzilishi wa kundi la muziki wa hip hop na rap maarufu kama Wateule. Pia anafahamika zaidi kwa kuimba maneno magumu na yenye vina vitata, sana-sana ni yeye na Fid Q.

 Ni mmoja kati ya wasanii wakongwe hapa nchini
Jay Moe akiwa ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la Wateule akiwa pamoja na akina Solo Thang, Jafaray, Mchizi Mox na Simba(R.I.P) pamoja na Kelvin ameweza kufanya vizuri na kukonga nyoyo za mashabiki huku wimbo wake uliomtambulisha kama Solo Artist ukiwa “Majukumu”.
Jay Moe amekuwa ambaye amekuwa akisfika kwa uhandishi makini na ideas tofauti, majukumu haikuwa mwanzo wa mwisho! Nyimbo kama Bishoo, Mvua na jua na Maisha ya Boarding zilimtangaza vyema katika tansinia ya muziki!

 

Wengi bado wanaamini “Ulimwengu ndiyo Mama” ya mwaka 2002 ndiyo albamu bora kupata kutokea hapa Tanzania kwa upande wa Hip hop. Ulimwengu ndiyo Mama ilisheheni vibao vingine kama Misosi, Mitungi na Pamba(Ay ), Safari njema(Dudu baya, Complex), Mpenzi kwaheri(TID), Ni mshamba(Sir Nature), Ulimwengu ndiyo mama rmx (Prof j)na Kama unataka demu(Q chief & Solo Thang).
Jay Moe kwa maneno yake mwenyewe anakiri kuwa hakufanya vizuri katika albamu yake ya pili. Hii iliwavunja moyo mashabiki wake wengi . Katika albamu kulikuwa na vibao kama Kasimama peke yake(Banana), Mwingine(Raha P) na Twende kwa mganga!!
Licha ya kutofanya vizuri katika albamu ya pili, Jay Moe hakulala na kukata tamaa, aliendelea kuitumia vizuri mikono ya P.Funk(Bongo Records) na Marco Chali(Kama kawa records). Mawe kama Story 3, Kimya Kimya, Cheza kwa Step(Ngwea), Tingisha(TID), Sihitaji(Lord Eyes) na baadaye Famous(Pfunk) zilizidi kuzihirisha uwezo wake.
Jay Moe akijiita  Mo-Techniques amekuwa kimbilio la wasanii wengi katika kutaka kuzifanya kazi zao zifanye vizuri, nyimbo kama Jirushe ya Feruz original version haikufanya vizuri kama Remix yake ambamo Jay Moe aliingiza verse yake, vivyo hivyo Nikipata wangu ya K-lyn ilikuja kufanya vizuri baada ya Jay Moe kuingiza sauti yake.
Jay Moe anakiri kuwa na urafiki wa karibu sana TID na umepelekea kufanya kazi kwa pamoja kwa miaka mingi. Kazi walizowahi fanya pamoja ni Zeze, Girfriend, Burudani, Mpenzi kwaheri, Tingisha na kazi ya karibuni kabisa ikiwa inaenda kwa jina la Chumvini!!
Mwisho niseme wasanii aina ya Jay Moe kwa miaka hiyo walijitambulisha kwa ubunifu na kujitengeneza wao kama wao. Kama ni Jay Moe utamsikia Jay moe tu, kama ni Solo thang basi ni Solo Thang tu na Prof J alikuwa ni Prof J peke yake!
mbali na apo jay mo ni msanii mojawapo mzuri ambaye katika kipindi chake cha kuimba muziki amepata tuzo moja tuu ya collabo ya ukisiki paa aliyoshirikishwa na JCB.
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *