LifeStyle

Maarifa 4 ambayo unatakiwa kujua ili kufanikiwa katika unachokifanya.

on

 

1. Sikiliza: fanya iwe silaha ya mawasiliano kwako.

Watu wengi huwa wanatumia mawasiliano mazuri pindi wanapoongea na kikundi cha watu, njia nzuri ya kutengeneza uaminifu kwa mtu ni kwa kuonyesha mvutu kwake ni njia nzuri ya kuleta mvuto huu ni kumsikiliza pindi anapokuambia kitu. wasikilizaji wazuri huwa hawafikirii wataongea nini baada ya muongeaji kumaliza kuongea.

2. Kuwa mwajibikaji; fanya ambacho umesema utafanya.

Pindi ambapo kitu kinaenda tofauti na ulivyo fanya usikichukulie mzaha, usikidharau wala usimlaumu mtu aliyekifanya hicho kitu cha zaidi tumia majukumu yako na uwajibikaji wako kuhakikisha kwamba umesahihisha hilo kosa na mambo kwenda sawa.

3. Ubunifu; tumia rasilimali ulizonazo.

Pale ambapo tatizo limetokea fanya juu chini kulitatua kwa kutumia maarifa na vifaa ulivyo navyo, tumia hasara ulipata katika faida uliyonayo, lenga vifaa ulivyonavyo sana kuliko vile ambavyo hauna.

4. Ufahamu wa hisia; jua na elewa hisia zako.

Pale ambapo unakuwa na siku nzuri au mbaya jitahidi sana usitoke katika hisia zako za kawaida japokuwa linaweza kuwa ni changamoto kubwa kwako kufanya hili jambo, ukweli ni kwamba pale ambapo unakuwa na hofu huonyesha uoga pia pale ambapo unakuwa na huzuni huonyesha hasira pia ukiwaa na hasira huwa mkimya mwenye huzuni cha msingi ni kuongea na wenzako na kutafuta mawazo chanya.
Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *