Health&Food

UFAHAMU UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA

on

Kifafa cha mimba ni ugonjwa ambao hutokea kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua. Ni ugonjwa hatari sana kwa mwanamke.

Viashiria ambavyo huwa vinaonyesha kwamba mama anakifafa cha mimba ni;

 

 • Shinikizo la damu
 • protini kuonekana kwenye mkojo pale unapopimwa
 • kupata degedege
 • Kuvimba miguu
DALILI HATARISHI ZINAASHIRIA KIFAFA CHA MIMBA NI;
 
 • Kichwa kuuma sana.
 • Kuona maruerue
 • Sehemu za tumbo kuuma
VISABABISHI VYA KIFAFA CHA MIMBA
 
 • Sababu haswa haijilikani
 • Kuwa na kipato cha chini
 • Unene uliopitiliza
 • Kurithi katika familia
 • Kuwa na ugonjwa wa shinikizo la damu
 • Kuwa na ugonjwa wa figo
 • Kuwa na ugonjwa wa kisukari
 • Kujifungua zaidi ya mara moja.
MATIBABU YA KIFAFA CHA MIMBA
 
 • Magnesium sulphate hii dawa husaidia kupunguza kile kitendo cha degedege kutokea mara kwa mara.
 • Diazepam hii husaidia mama kupata usingizi na kupumzika pale ambapo amepata degedege
 • Hydrocortisone hii ni dawa ambayo husaidia moyo kuendelea kufanya kazi vizuri
 • Hydralazine hii ni dawa ambayo hushusha pressure

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *