Inspiration

Kanuni kumi za mafanikio kutoka kwa Adamu Mchomvu( Baba Johniii!!!)

on

 

Ni msanii wa miondoko ya Hiphop pia ni mtangazaji Alipata kazi Clouds Fm baada ya mashindano ya kutafuta mtangazaji wa Africa bamba taa walikuwa zaidi ya mia ila alipita anafanya vipindi vya Soso fresh ya clouds Fm pia xxl ya clouds Fm ni mbunifu wa maneno ya mitaani sana soma kanuni zake kumi za mafanikio hapa

1.Fanya unachokipenda
Nikiwa Uganda kwenye masomo nilipenda sana mziki hivyo nilikuwa ninahost matamasha mbalimbali katika shule yetu.

2. Tafuta njia yako
Sishangai watangazaji wengine kuniiga jinsi ninavyotangaza ila ni muhimu sana kutafuta njia yako au namna yako mwenyewe ya kufanya kitu.

3. Ongeza maarifa
Nasoma vitabu ili kuhakikisha naongeza maarifa hii itanisadia kujua vitu vingi kiundania zaidi ni vyema kujua vitu nje ya Box

4. Tumikia kazi uliyochagua
huwa napigiwa simu mara kwa mara na wasanii mbalimbali mpaka inaboa ila navumilia kwa sababu ndiyo kazi niliyochagua.

5. Pambana mwenyewe
Watoto wa uswahilini wanapambana wenyewe ili kuonesha kwamba hata wao wanauwezo wa kutoa maisha hata kama siyo watoto wa kishua.

6. Piga hatua ili utoke sehemu ambayo hupendi kuwa katika maisha yako.

7. Kuwa mbunifu

8. Tengeneza urafiki na watu ambao wanapenda unachokifanya.

9. Sikiliza moyo wako

10. kila kitu kinawezekana

 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *