Inspiration

Kanuni kumi za mafanikio kutoka kwa nguli wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya “AY”

on

 

1. penya kwenye uwezo wa kupenya;

Nilikuwa sina mawasiliano yeyote katika nchi ya Kenya ila pale ambapo nilipata mpenyo wa kupata interview Kenya huo ndio ulikuwa mwanzo wa kupenya vizuri katika soko la muziki Africa.

2. Jiamini;

Mimi nakukumbuka tukiwa katika tuzo za Mtv Mama Africa Akon alikuja akiwa kwa mbele yetu wasanii wenzangu waliogopa kukutana naye mimi sikuogopa nikajiamini nikamwita hey Kon akashutuka akaniface tukapiga naye story. Mimi huwa siogopi najiamini kwa kitu ninachokifanya.

3. Pambana;

Mimi muda mwingine nasafiri kwenda Marekani huko nchi za watu sijui mtu saa zingine utanikuta kwenye mashamba huko napambana haswaa na maisha.

4. Shindana;

Kipindi kile sisi tunaanza muziki watu walikuwa wanajua kweli ushindani ulikuwa mkubwa kwa hiyo nilikuwa nafanya juu chini ili niweze kushindana vyema na wenzangu.

5. Jitengeneze;

Nilianza muziki mwaka 1996 ila nilijulikana rasmi mwaka 2000 ikiwa na maana baada ya miaka sita ndiyo Bongo fleva ilinitambua Rasmi muda wote huo nilikuwa najitengeneza vizuri.

6. Nyumbuliza;

Jina la mzee wa commercial nilipewa na P Funk kwa sababu alikuwa akinipa beat ngumu naweza kuchana, akinipa beat ya ragger tone naweza kupita vizuri kabisa yaani mpaka yeye akanikubali Beat yeyote napita hii ni kwa sababu nilikuwa flexible.

7. Fanya vitu tofauti;

mimi nanakipindi cha tv cha Mkasi pia najishughulisha na shughuli za shamba huku nipo kwenye muziki hii inafanya kuingiza hela katika vitu tofauti.

8. Jitume sana

9. Kuwa na mipango

10. Kila kitu kina hatua tengeneza mtandao

Kanuni hizi zimeandaliwa kwa kusikiliza mahojiano mbalimbali ya msanii huyu katika vipindi mbalimbali hasa hasa Mkasi TV show na The avenue mawazohuru

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *