Inspiration

Kanuni kumi za mafanikio kutoka kwa Dr. Reginald Mengi.

on

 

1. Umasikini ni changamoto na siyo tatizo

“Tatizo hukaa juu ya mabega yako na kukushindilia chini wakati changamoto hukaa mbele yako na wewe kuanza kupambana dhidi yake”.

2. Jione wewe mwenyewe ni mshindi

“Washindi katika dunia hii huona vitu katika jicho la changamoto, maisha kwa ujumla ni tofauti kulingana na wewe unavyoyaona maisha”

3. Mwamini Mungu

“Kama ukiamini katika jina la Mungu na Nguvu za Mungu utaona kila kitu ni tofauti na utakuwa na hamasa ya kufanya, kufanya, kufanya”.

4. Jiamini

“Jiulize unataka kufanya nini Amini unaweza kufanya amini unaweza kuweka nguvu zako na ukatengeneza kitu”.

5. Sema ndiyo naweza. lazima nifanye.

“Nilikuwa sina mtaji wowote nimewahi kuamka mfukoni sina hela kisha nikasema naweza kufanya “.

6. Fanya kazi kwa bidii.

“Usifanye kazi kirahisi, kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii,”

7. Anza kidogo ili fikiria kwa ukubwa.

“kuanza kidogo ni asili ya kupata kikubwa, siku zote ukiwa unaanza jua unakoenda pale ambapo utajua unaenda wapi hapo ndipo utaweka mipango.Pangilia safari yako, lazima ujue wapi unaenda usiende na kurudi kwa sababu ukienda na kurudi mwishoni maisha yako yatakosa mpangilio”.

9. Kuwa wa kwanza.

“Jipe namba moja mwenyewe, usijibe nafasi ya pili, jiweke katika nafasi za juu na jione unadhamani kubwa kwa sababu nafasi ambayo utajipa mwenyewe hakuna ambaye ataweza kuichukua.”

10. Mpe mtu kazi yako kwa kujiamini.

Usimwamini mtu nusu, kama huwezi kumpa mtu kazi yako huwezi kutanuka kibiashara na kupata mafanikio.”

10. Shukuru na toa

“Mshukuru Mungu pamoja na watu waliokufanya wewe ukawa tajiri, pesa zangu zinatoka kwa wote masikini na tajiri saidia jamii”.

Zimekusanywa kwa kusikiliza mahojiano mbalimbali ya Dr. Reginald Mengi.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *