Inspiration

Kanuni kumi za mafanikio kutoka kwa Ben Paul

on

 

Msanii huyu kutoka Mji wa Dodoma ambaye anafanya vizuri sana na ngoma yake ya Phone amewahi kufanya ngoma kali kama moyo mashine, jikubali, na nyingine nyingi hivyo kumfanya awe msanii ambaye ameweza kufanikiwa sana katika mziki wa Bongo Fleva katika mahadhi ya R&B. HIzi ndizo mbinu zake za mafanikio

1. Bidii

2. Kusaidiana

3. Nidhamu

4. Kuwa na mawasiliana na watu wanaofanya vitu vinavyofanana na vyako.

5.  Amini unachokifanya kinaweza kukusaidia
Alimwambia baba yake amesitisha chuo ili kufanya muziki kwa sababu ndio kitu anaamini kinaweza kumsaidia.

6. Jikubali
Baada ya mdogo wake kufeli form four aliamua kutunga nyimbo jikubali ili kumwambia kwamba anaweza kufanya chochote na akafanikiwa ajikubali tuu.

7. Pumzika
Huwa muda mwingine natoka naenda zanzibar kupumzika muda mwingine ni muhimu kuwa nje ya kazi.

8. Usiwe na hofu
Sina hofu sofia nilitoa wakati nyimbo nyingi zinafanyiwa nje ya nchi zimetoka ila sofia ilifika mbali sana hii ni kwa sababu sikuogopa.

9. Penda kitu unachokifanya
Kila siku najitahidi kuongeza kitu katika kitu ninachokifanya kwa sababu nakipenda kutoka moyoni.

10. Kila kitu kinawezekana
mimi najiona nipo hapa kwa sababu naamini kila kitu kinawezekana kwa uwezo wa Mungu.

Kanuni hizi zimeandaliwa kwa kusikiliza mahojiano ya msanii huyu katika kipindi cha The Avenue Mawazo huru

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *