Health&Food

Jinsi ya kuendelea kuwa na afya bora wakati wa ujauzito

on

Mama na mtoto wake wanaweza kuendelea kuwa na afya bora kwa:

 • Kupata chakula cha kutosha chenye virutubishi.
 • Kupumuzika sana kila siku.
 • Kuepuka kemikali, pombe, moshi, na sehemu kubwa ya madawa.
 • Kupata huduma kutoka kwa mkunga au mfanyakazi wa afya mwingine
  ambaye anaweza kutibu, au kusaidia kupata matibabu kwa ajili ya tatizo
  lolote la kiafya ambalo linaweza kujitokeza.
 • Upendo na huruma.

Kula chakula cha kutosha chenye virutubishi

Mchanganyiko wa chakula chenye virutubishi kitamfanya mwanamke awe na
nguvu na afya; aweze kupata nguvu za kujifungua na kumhudumia mtoto.
Kama mwanamke mjamzito hali chakula cha kutosha, inawezekana anawachia
chakula wana familia wengine, au mama mkwe kwa nia njema katika uelewa
wake amemwambia asile baadhi ya vyakula au asiongezeke uzito ili aweze
kujifungua kwa urahisi. Kumbuka mwanamke analazimika kula chakula cha
kumtosha yeye na mwanae. Hivyo anahitaji kula chakula zaidi kuliko watu
wazima wengine na siyo kidogo kuliko wao.

Wanawake wajawazito, kama watu wengine, wanahitaji mchanganyiko
wa protini, mbogamboga,matunda, na wanga. Pia wanapaswa kula mara nyingi
zaidi, wakipata vyakula vidogo vidogo kati ya milo ya kawaida siku
nzima. Kwa ushauri kuhusu ulaji bora, angalia Lishe bora hutengeneza afya bora.

Vyakula mchanganyiko hulinda afya ya mama na mtoto.

Zuia upungufu wa chembe nyekundu za damu (anemia)

Anemia
(upungufu wa chembe nyekundu kwenye damu) hutokea sana wakati wa
ujauzito. Husababisha kujisikia mchovu kila mara. Anemia ni hatari zaidi
hasa kwa akinamama wajawazito kwa sababu damu hupotea wakati wa
kujifungua. Hii inaweza kuzidisha upungufu huo na kusababisha mama
kupoteza maisha. Zuia anemia kwa kula vyakula vyenye protini na wingi wa
madini chuma, na pia kutumia dawa ya kuongeza madini chuma mwilinikwa ajili ya taarifa zaidi juu ya madini chuma na njia zingine za ziada za kuongeza madini chuma mwilini.

Malaria (angalia Baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukiza (kinaandaliwa) na minyoo ya safura) vinaweza kusababisha anemia na hivyo hutakiwa kutibiwa mara moja.

Akina mama wajawazito wanahitaji vyakula vyenye wingi wa madini chuma.

Tindikali ya Foliki

Ukosefu wa tindikali ya foliki (au vitamini ya foleti) kunaweza
kusababisha hitilafu katika umbaaji wa mtoto na hata ulemavu. Chagua
dawa za kuongeza madini chuma mwilini ambazo zinajumuisha tindikali ya
foliki, au dawa za kuongeza foliki mwilini.

Vitamini A

Mbogamboga za kijani na matunda ya rangi ya chungwa huwa na vitamini A,
kirutubishi ambacho kinahitajika kwa ajili ya afya ya macho. Mwanamke
mjamzito anahitaji mbogamboga za kijani na matunda ya rangi ya chungwa
zaidi kwa sababu vitamini A anayokula hutumika kwanza kukidhi mahitaji
ya mtoto. Ukosefu wa vitamini A unaweza kusababisha kutoona usiku au upofu kwa ujumla.

Kupumzika

Wahimize wanafamilia na majirani kumsaidia mama mjamzito katika kazi
na majukumu yake. Mkumbushe, hasa ujauzito unapozidi kukua, kupumzika na
kuinua miguu yake juu mara kadhaa kwa siku au kulala chini wakati wa
alfajiri. Kulea ujauzito ni kazi kwa mwili; nao mwili unahitaji
kupumzika.

Epuka Matumizi ya Bidhaa Hatari

Usivute sigara ndani rafiki yangu, dada yangu ni mjamzito!

Moshi na sigara

Sigara na tumbaku huathiri mapafu ya mama na vinaweza kusabisha
saratani na hata kifo. Moshi unaweza kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya
muda wake au akiwa na uzito mdogo sana, au akiwa amekwisha kufa. Akina
mama na watoto wao wanaweza hata kudhurika kutokana na watu wanovuta
sigara karibu nao. Ikumbushe familia na wengine kuepuka kuvuta sigara
katika chumba kimoja au kweye gari wanapokuwa na mama mjamzito au
watoto.

Pombe na madawa ya kulevya

Mama mjamzito anapokunywa pombe, pombe hiyo huenda kwa mwanae na
inaweza kusababisha hitilafu za kudumu kwenye ubongo wa mtoto na mwili
wake. Kadri anavyozidi kunywa pombe nyingi ndivyo madhara kwa mtoto
yanavyongezeka. Vivyo hivyo, madawa ya kulevya yakiwemo kokeni, bangi,
unga na madawa mengine ni hatari kwa akinamama wajawazito na watoto wao.
Angalia Madawa ya kulevya, pombe na tumbaku (kinaandaliwa) kwa msaada zaidi juu ya madawa na pombe.

Madawa ya kawaida

Dawa nyingi anapozitumia mwanamke mjamzito pia humfikia mtoto wake.
Kwa sababu watoto tumboni wanakuwa wadogo sana na wakiendelea kuumbika,
dawa ambazo ni salama kwa mtu mzima zinaweza kusababisha hitilafu wakati
wa kujifungua na hata madhara kwa mtoto. Hivyo akina mama wajawazito
wanapaswa kuepuka kutumia dawa holela. Kupumzika na vinywaji laini —
siyo dawa — ndiyo tiba bora zaidi kwa matatizo madogo madogo kama vile
maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, na mafua.

Isipokuwa tu kama una uhakika yanahitajika, ni bora zaidi kuepuka madawa wakati wa ujauzito.

Lakini baadhi ya magonjwa ni hatari sana kuyaachia bila kuyatibu
katika kipindi chote cha ujauzito. Ugonjwa unaweza kuwa hatari pia kwa
mtoto. Magonjwa kwa wanawake wajawazito ambayo yanapaswa kutibiwa na
dawa ni pamoja na:

 • malaria. Angalia pia Baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukiza (kinaadaliwa).
 • VVU na UKIMWI. Angalia VVU na UKIMWI (kinaadaliwa).
 • maambukizi ya njia ya mkojo. Angalia pia Matatizo katika utoaji mkojo (kinaadaliwa).
 • maambukizi kupitia ngono kama vile klamidia, kisonono, na kaswende. Angalia pia Matatizo na maambukizi ya via vya uzazi (kinaandaliwa).

Ili kujua iwapo dawa yeyote ile ni salama kutumia wakati wa ujauzito
na wakati wa unyonyeshaji, muulize mfanyakazi wa afya mwenye uzoefu.
Angalia pia sehemu ya dawa mwishoni mwa sura hii, au rejea miongozo
mingine juu ya matumizi ya dawa. Kwa dawa ambazo zinahitajika lakini
siyo salama, kawaida huwa kuna dawa nyingine mbadala ambayo inaweza
kutumika.

Dawa za asili na mimea/mitidawa zinaweza kusababisha madhara zaidi kuliko kutoa tiba. Kitabu kiitwacho Dawa, vipimo na matibabu (kinaandaliwa) kimependekeza njia za kuzingatia unapotaka kufanya maamuzi juu ya matumizi ya dawa za asili.

Epuka kukutana na wagonjwa

Kuugua wakati wa ujauzito ni taabu kubwa. Ugonjwa unaweza kusababisha
taabu kubwa katika kula, na kutokula chakula cha kutosha humunyima
mwanamke mjamzito nguvu. Epuka kukutana na wagonjwa kupunguza uwezekano
wa kuambukizwa.

Ugonjwa wa Rubella ambao ni aina ya surua kawaida siyo hatari sana.
Lakini unapompata mwanamke mjamzito unaweza kusababisha hitilafu katika
viungo na hata ulemavu kwa mtoto akiwa tumboni. Katika kumlinda mtoto,
mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka watu wenye upele, hasa watoto, ambao
mara nyingi hupatwa maambukizi hayo. Hata watoto wengine wa mama
mjamzito ambao wanaumwa wanapaswa kuhudumiwa na wanafamilia wengine au
marafiki. Kampeni ya chanjo kwa jamii nzima ndiyo kinga bora zaidi kwa
wanawake wote.

Huduma ya mkunga au mfanyakazi mwingine wa afya

Mkunga mzoefu au mfanyakazi wa afya mwingine anaweza kumshauri
mwanamke mjamzito jinsi ya kuishi na afya nzuri na salama, kutibu
magonjwa yote ya kawaida na kupunguza kero, na kutambua lini mwanamke
mjamzito anapohitaji kutafuta msaada kwenye hospitali au kituo cha afya.
Wanawake wote wanapaswa kuhudumiwa na mfanyakazi wa afya mwenye huruma
na ueledi wakati wa ujauzito, pale wanapojifungua na katika wiki
zinazofuata.

Chanjo

Mwanamke mjamzito anapaswa kuchanjwa dhidi ya pepopunda (tetanasi)
mapema iwezekanavyo katika ujauzito. Anatakiwa kupewa chanjo nyingine
wiki 4 baadaye iwapo atakuwa hajapata chanjo zote. Hii husaidia
kuwalinda wote wawili-mama na mtoto wake. Kwa taarifa zaidi angalia Chanjo (kinaandaliwa).

Vipimo vya Maabara

Vipimo rahisi vinaweza kugundua baadhi ya magonjwa mengi ambayo ni
hatari kwa wanawake na watoto wachanga. Vipimo hivi huwatahadharisha
mama na mfanyakazi wa afya kuanza matibabu mara moja, hatua ambayo
inaweza kuzuia matatizo makubwa wakati na baada ya kujifungua. Ni busara
kufanya vipimo dhidi ya:

 • anemia (kwa kutumia kipimo maalum cha himoglobini).
 • kaswende.
 • malaria (kwa kutumia vipimo ambavyo hutoa majibu haraka kwa maeneo ambapo malaria ni ugonjwa wa kawaida).

Kipimo cha VVU kinatakiwa kutolewa kwa akina mama wote wajawazito. Mwanamke anapogundua ana VVU, anaweza kuanza kutumia dawa ya kumsaidia afya yake na kumlinda mtoto asiambukizwe VVU. Sura ya VVU na UKIMWI (kinaandaliwa) inajumwisha taarifa juu ya upimaji na dawa ambazo wanawake wajawazito wenye VVU wanapaswa kutumia.

Kuna aina mpya ya vipimo vya VVU ambavyo havihitaji maabara na
hufanyika kwa urahisi kwa kutumia kifaa kidogo kupangusha ndani ya mdomo
au ukeni, au kuchukua tone la damu kutoka kwenye tundu dogo kwenye
kidole. Ulizia kwenye kituo cha afya kilichoko karibu iwapo vipimo hivi
hutolewa na serikali, au kama kuna shirika lolote ambalo linatoa huduma
hiyo.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *