Cellebs

Mfahamu kwa undani Ruge Mutahaba

on

Amezaliwa  Brooklyn New York Marekani mwaka 1970 shule ya primary nimesoma Arusha school darasa la 1 hadi la 6 kisha nikahamia Mlimani primary school maeneo ya chuo kikuu Dar es salam ndipo nilipomaliza la saba. Kisha nikasoma Forodhani secondary school o -level na Pugu high school a-level. Baada ya hapo nilirudi marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University Carliphonia  ambako nilichukua masomo ya BA in  marketing  pia nikawa nachukua BA in finance kozi zote nilisoma mdani ya miaka mitano. Baada ya hapo nikarudi bongo

KUANZISHA CLOUDS ENTERTAINMENT…. “Wakati nipo Marekani  JOSEPH KUSAGA alikuwa na disko linaloitwa clouds disko. Mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya miziki then hapo tukatengeneza urafiki. Sasa niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, JOSEPH KUSAGA akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio ndipo nikajikuta nipo clouds entertainment.

KUANZISHA T.H.T….. Kama Clouds entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya managment ya wasanii ambayo tuliita smooth vibes ambayo ndivyo kampuni iliyowatoa wasanii kama Ray c na Jay Dee. Pia tulianzisha TANZANIA HOUSE OF TALENT ambayo sasa kupitia hiyo tukawa tunawafundisha wasanii how to manage industry, music business, music instrumentation and dance classes THT imewatoa wasanii kama Barnaba, Marlaw, Linah n.k

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *