Cellebs

Mfahamu harmonize alipotoka na harakati zake kimaisha

on

 

Harmonize amezaliwa mwaka 1992 huko mkoani Mtwara ,Akiwa ametoka Dar akiomba kupafomu katika tamasha la fiesta katika mkoa wa Mtwara shoo ilichelewa kwa sababu ya kuwa na mchezo wa mpira wa miguu na alipanga chumba karibu na uwanja akiwa amelala alisikia Fid Q anapafomu ile anatoka tuu alikutana na vibaka na kunyang’anya vitu vyote. hivyo alishindwa kupafomu.

Akiwa anarudi Dae es Salam presenter mmja alimuonea huruma na kuamua kumpa namba ya DIAMOND kwa sababu HARMONIZE alikuwa amekata tamaa hakutaka hata kumpigia Diamond kwa sababu hakujua ataanzia wapi.

Akiwa nyumbani aliokota simu  ya watssp na akaona profile ya Diamond kwenye simu yake hakuamini mpaka pale alipoona amebadilisha profile ya kuweka picha ya Zari. Alimtumia massage ya kujitambulisha pamoja na nyimbo yake moja.

Alimuomba Diamond amsindikize katika shoo ambayo atafanya DAR LIVE alimwambia haina shida atamuombea Harmonize atangulie kaba yeye apafomu. Diamond alimwambia Harmonize kwamba achukue namba ya Brother D ili awasiliane na yeye.

HARMONIZE alipata nafasi ya kupafomu katika hiyo shoo ya DAR LIVE na kumuomba Rafiki kuchukua video katika simu yake na baadaye usiku alimtumia Diamond ile video  na kumshukuru kwa hiyo nafasi.

Diamond alimuuliza kama ana managment akamjibu hana na huo ndio  ukawa upenyo wake. BROTHER D aliamuambia atunge nyimbo inahusu foleni. Alitunga na kumtumia Brother D alimkubali sana.

Alichukua ngoma yake na kupeleka CLOUDS FM   walimkubali sana na kumpa namba ya ADAM MCHOMVU ili aweze kuongea naye kwa ajili ya kuitambulisha hiyo nyimbo katika kipindi cha BONGO FLEVA. Alifanikiwa kuitambuisha hiyo ngoma.

Diamond alimchukua na kumpeleka WCB  kuishi huko kwa sababu mazingira yake ya kuishi yalikuwa magumu na kuishi naye kama mdogo wake. Alisainiwa WCB na kufanya kazi ya AIYOLA ambayo video yake imefanyika katika nchi ya SOUTH AFRICA na kufanya vizuri.

Mwaka 2016 alifanikiwa kunyakua tuzo mbili ambayo ni msanii bora chipukizi Africa katika tuzo za AFRIMMA pia nyimbo yake ya Bado ulishinda tuzo ya nyimbo bora ya kushirikishwa huko Ghana. 2017 penzi lake lilikolea kwa Jackline Wolper hadi kufikia hatua ya kutoa Ngoma yake ambayo Wolper alitumika kama video queen.

 

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *