Uncategorized

JE UNAJUA MNYWAJI WA POMBE ANAWEZA KUPATA MATATIZO ZAIDI YA 10?

on

 Watu wengi hupenda sana kunywa pombe kama kiburudisho pia wengine hupenda kunywa pombe kama njia ya kupunguza shida zao au kusahau yale amabayo wametendewa na dunia au watu wanaoishi duniani. ila mara nyingi huwa hawakumbuki kwamba mathara ya unywaji wa pombe ni makubwa kushinda hata faida zake. yafuatayo ni madhara ya pombe katika mwili wa binadamu.

UGONJWA WA AKILI(PSYCHOSIS) 

huu ni ugonjwa ambao hutokea pale ambapo pombe inafika hadi kwenye ubongo na kuharibu sehemu ambayo inahusika na njia ya mawasiliano huu uharubifu unaweza kusababisha mudi ya mtu ikaharibika na tabia yake pia ikawa mbaya mfano anaweza kuanza kupiga watu na kuvunja vitu pia kuongea maneno ambayo hayaeleweki kumumunya maneno.

STROKE( CEREBRAL VASCULAR ACCIDENT)

Huu na ugonjwa ambao unaweza kusababishwa na unywaji wa pombe kwa sababu pombe huadhiri mishipa ya damu pamoja na moyo hivyo kusababisha mzunguko wa damu mwilini kuwa wa shida hadi kupelekea ubongo kukosa damu ya kutosha kisha kusababisha hewa safi ya oxygen kokosekana katika baadhi ya sehemu za ubongo hivyo mtu kupooza au kuanguka ghafla.

SHINIKIZO LA DAMU(HYPERTANSION) 

Huu hutokea pale ambapo pombe inaenda kusababisha moyo kusukuma damu kwa kasi pia kufa nyafanya mishipa ya damu kuwa nyembamba hivyo kusababisha damu kutoka kwa kasi sana na moyo kusukuma damu kwa nguvu ili kuweza kuisambaza katika sehemu mbalimbali za mwili.

MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (HEART FAILURE)


Hii husababishwa na pombe kuchokesha misuli ya moyo hivyo moyo kushindwa kusukuma damu kwenda kwenye sehemu mbalimbali za mwili hivyo kusabisha damu ibaki mwili na maji kujaa katika srhemu mbalimbali za mwili hasahasa miguuni na kwenye mapafu.

INI KUFELI(LIVER CIRROSIS) 


Hii hutokea pale ambapo mtu anakunywa pombe kupita kiasi na kwa kawaida kazi ya kuondoa sumu mwilini hufanywa na ini sasa pombe ni sumu kwa hiyo kinachotokea ni kwamba ini linashindwa kutoa sumu ndani yake baada ya pombe kuzidi na hivyo kulisababisha liwe na makovu na lishindwe kufanya kazi hivyo kupelekea tumbo kuvimba kukosa hamu ya kula pia miguu kuvimba na kutapika nyongo.

HOMA YA INI( HEPATITIS)


Hii hutokea pale ambapo mtu anakunywa pombe kupita kiasi hadi ini linazidiwa na hivyo ssli zake kuanza kufa dalili ya kwa ni kuwa na rangi ya njano katika sehemu za jicho na kwenye ngozi. na kukosa hamu ya kula.

SARATANI YA MAPAFU(LUNG CANCER) 


Hii hutokea pale ambapo mtu anakunywa pombe kupita kiasi na kusababisha pombe kubadilisha ukuaji na utengenezaji wa seli zake za mwili na kuanza kujitengenezea seli mpya ambazo baadaye huwa hazifi na kutengeneza uvimbe ndani ya mapafu .

SARATANI YA KOROMEO( OESOPHAGUS CANCER)


Hii pia husababishwa na unywaji pombe kali kama viroba gonga wiski na konyagi hizi huchubua koo la hewa kwa sababu zina acid kubwa na kusabaisha uharibifu wa ukuaji wa seli ndani ya koo la chakula hivyo kupelekea mtu kukosa hamu ya kula pia kushindwa kumeza chakula.

VIDONDA VYA TUMBO ( PEPTIC ULCER DISEASE) 


Kwa kawaida pombe ina asili ya tindi kali yaani acid na ndani ya tumbo hutengenezwa hydrocloric acid ambayo kazi yake ni kumeng’enya chakula sasa kinachotea kwa mlevi kawaida huwa hapendi kula hivyo kusababisha pombe pamoja na hii tindi kali ndani ya tumbo kuanza kukwangua tumbo na kuleta vidonda.

KUWA HANISI (IMPOTENCE)

hii ni kwa upande wa wanaume ambapo mwanaume anashindwa kusimamisha au akisimamisha uume wake anashindwa kufika kileleni hii ni kwa sababu ya kutopenda kula pia pombe hulegeza misuli ya via vya uzazi na pia huaribu msukumo wa damu hivyo mwanaume kushindwa kumridhisha mke au mchumba ake.

UGUMBA( INFERTILITY)


maelezo yake ni sawa na hapo kwa mwanaume.
MATATIZO YA KIJAMII NAKIUCHUMI KAMA VILE 


migogoro ndani ya familia,uchumi wa familia kuyumba, kutengwa na jamii, kuharibu malengo yako ya maisha na kugombana ovyoo.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *