Uncategorized

HISTORIA YA JOH MAKINI

on

Huyu ni kijana wa kwanza katika familia ya simon mseke alianza muziki miaka ya 1995 katika jiji la Arusha akiwa mara nyingi akifanyia nyimbo zake noise makers studio iliyoko arusha. kwahiyo ndani ya muziki huu anamiaka kama 20 hivi katika gemu ya bongo fleva.

NENO Bongo fleva husimama kumaanisha aina ya muziki wa kizazi kipya unaofanya na wasanii wa kizazi kipya,hususani vijana huku wengine wakitumia staili za kughani(kurap) na wengine wakiimba kwa lugha za kiswahili.
Katika hili limekuwa likizua utata kwa baadhi ya wasanii wakikataa kujumuishwa kwenye majina ya wasanii wa Bongo fleva kwa kile wanachodai kuwa waowanafanya Hiphop na sio Bongo fleva na kuacha utata mkubwa huku baadhi ya mashabiki na wadau wakiwa hawajui kutofautisha kati ya Bongo fleva na Hiphop.
Msanii tuanae muangalia leo ni mmoja kati ya anayefanya aina ya Hiphop na sio Bongo fleva,hili ni kutokana na aina za midundo na dhamira zinazopatikana kwenye nyimbo zake pamoja na aina anayoitumia katika mwenendo wa maisha yake.
Huyu sio mwingine bali John Simon Mseke anayejulikana zaidi kama ‘Jo makini’, msanii anayetokea Mkoani Arusha ambaye yeye mwenyewe kwenye nyimbo zake hupenda kujitambulisha kwa jina la mwamba
wa kaskazini.
Kwa hivi sasa hapa nchini unapowataja wasanii wanaofanya Hiphop hapa nchini,Jo makini ni mmoja kati ya wanahiphop ambao wapo juu kileleni akifanya vizuri na nyimbo yake inayotamba kwa hivi sasa inayokwenda kwa jina la NUSU NUSU imepikwa na nareel na video yake kufanyika south afrika na kufika nafasi hadi ya nane katika channel na mtv africa.JOH MAKINI  anatokea sinoni daraja mbili ambako ndiko alikonzia muziki wake kama kikundi kinachoitwa RIVER CAMP SOLDIERS akiwa pamoja na wasanii kama Bonta, mdogo ake Nikki wa ii pamoja na Stooper rhymers. Mbali na hapo mwamba wa kaskazini pia amekuwa akifanya kazi zake kama solo artist.

Joh makini ametoa nyimbo kama mfalme, wameinama, stimuzimelipiwa , zamu yangu, chochote popote katika miaka ya 2000 mpaka 2012. 
katika miaka hiyo joh aliweza kushinda tuzo ya nyimbo bora ya hiphop katika tuza za KTMA  kwa  nyimbo ya stimu zimelipiwa.

Katika miaka ya 2010 kuendelea kikundi cha river camp pamoja na kikundi cha nako 2 nako viliungana na kutengeneza kampuni inayoitwa WEUSI. kazi ya hii kampuni ni kusimamia kazi zote za wasanii waliopo chini ya lebel hii. kutoka hapa joh makini alibadilika na kuanza kutoa video kali ambazo zilikuwa zina ubora kulingana na muziki unavyoenda.

Video hizo ni kama manuva, karibu kwenye show za joh, OX pamoja na NUSU NUSU. Kwa sasa inaonekana kwamba joh anatakataka kupenya soko la nje kwa sababu anajitahidi sana kufanya video kali na ngoma kali na anampango wa kufanya ngoma na rapper kutoka Afrika kusini aitwaye A.k.A.

mwaka 2015 ameshinda tuzo ya msanii bora wa hiphop na mwandishi bora wa hiphop 2014 katika tuzo za KTMA.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *