Cellebs

Mfahamu kiundani Nay Wa Mitego na harakati zake

on

Anaitwa Emmaunel Elbariki Munisi baba yake ni mchaga na mama yake ni mnyakyusa alianza harakati zake za muziki mwaka 1996 lakini kwa upende wake anasema haoni sababu ya kujiona mkongwe kwa sababu hajivunii kuanza muziki zamani.

Mwaka 1998 alirekodi nyimbo yake ya kwanza inayoitwa dala dala pia mwaka huo huo alitengeneza kundi lililoitwa wagod family nyimbo iliitwa enzayme lakini baaada ya muda kundi lilivunjika.

Mwaka 2000 alirekodi tena nyimbo yake nyingine katika studio za sound crafters kwa shilingi 17000 ambayo aliiba nyumbani ikamfanya mama amletee noma pia mwaka huo huo Ney alimaliza la saba na baada ya mama yake kuona kijana anapenda mzuki sana na kuumuuliza achague katika ya kusoma au kuacha muziki lakini yeye alitaka vyote hivyo kumfanya mama yake amfukuze nyumbani.

Baada ya kufukuzwa nyumbani alienda kukaa na kaka yake wa kitaa na kumuomba alale saluni kwake huku akimsaidia kufanya usafi saluni pia na kunyoa. Amesoma Mbezi beach secondary school na alikuwa akitegemea pesa ya nauli kwa saluni.

Akiwa kidato cha pili alianzisha mausiano ya kimapenzi na msichana wa kiarabu na kumpa mimba hiyo ilimfanya akimbie mjini na kujificha ili kuweza kuhuruhusu mpenzi wake ajifingue mtoto baada ya kujifungua alifukuzwa nyumbani na Ney kuamua kupanga Manzese kwa mfuga mbwa na kuishi nae. Baada ya hapo maisha yalikuwa magumu na kurejea kuishi nyumbani kwa huo mwanamke.

AKIWA FORM 2 alienda kurekodi nyimbo kwa majani ilikuwa inaitwa kama unanipenda ambayo hela ya kurekodia alichukua ada ya shule.Alikutana na bro anayeitwa John mjema na kutokea kumpenda Ney na kumuomba wafanye kitu. Na alimuona Ney atakuja kuwa mwalimu wa mahasla. John Mjema alikuwa anafanya kazi posta hivyo ney alikuwa anamfuata huko.

John Mjema limshauri asivute bangi wala madawa kwa sababu alikuwa anaishi Feri ambako wanakaa wahuni wengi John alikuwa anamsaidia sana kumpa hela ya kula alikaa feri kwa mienzi 6. John alipata matitizo na kufanya Ney arudi Manzese na kuishi tena saluni. Washkaji walimcheka sana na yeye kuamua maisha yake kuwa ya salon.

Ney alikuwa anatembea kwa mguu kwenda kwa P funk, Master Jay na Bonny Love anasema alikutana na mchizi wake na kumwambia twende wakaishi pamoja na kumwambia waishi kama ndugu aliikaa kama mwenzi. Siku moja akiwa amelala tena anaumwa alirudi saa saba tena na mwanamke akamwambia huyu ni mke wangu so nakiomba urudi saluni tena ukaishi mpaka utakapopata sehemu nyingine.

Ney anasema maisha magimu yote aliyopitia hajawahi kulia lakini siku hiyo alilia baaada ya kuchukua mfuko wake wa rambo na kuwaza kurudi nyumbani. katika safari alikamatwa na sungusungy na kupelekwa polisi siku hiyo hoyo. kesho jioni alitolewa na askari ambaye ni kaka wa msela aliyesoma nae.

Alirudi tena kwa bro wa saluni na kumuomba akae mpaka apate chumba tena baada ya hapo alipatakaziwa kesi na kukaa segereia kwa mienzi 3. Ney anasema kwamba aliacha bangi kiajabu kwani aliamka asubuhi tuu na kujikuta havuti.

Baada ya kutoka jela alitoa nyimbo inayoitwa Wa mitego chini ya p funk na anasema anapenda kuwa free na baada kutoa hito nyimbo ndio akapata jina Ney wa mitego kwa sababu watu waliomba nyimbo hiyo. Baada ya alihama Bongo record na kwenda kwa jar man kurekodi itafaamika hapa Ney aliweza kupanga na kumiliki ile saluni.

Alikuja kurekodi tena Hello ambayo ulibadilisha maisha yake na kuweza kulipwa laki nane kwa shoo moja anasema hakuamini. Hela hiyo ndio ikimfanya atoe video ya hello pia Alitoa ukwel wa moyo ambayo iliweza kumpa GX 100 alikuwa akiishi Sinza hapa Ney alikuwa siriazi zaidi na muziki

Baada ya hapo alitoa Nasema nao ambao ulimfanya apate mafanikio ya muziki sana na kufanya shoo na makampuni. Ney pia ni mshabiki wa Diamond na kwenda kwa shoo zake.

NEY alipata tuzo ya nyimbo bora kushirikiana ya Muziki gani na Diamond baadaye Nakula ujana kwa sasa NEY anamiliki nyumba mbili zenye hathi ya kisasa na zimemgarimu kiasi cha milioni 200 nzuri sana pia anafanya biashara mbalimbali. anamiliki nissani morano iliyomgarimu kiasi cha milioni 72. pia anabajaji mbili.

Nay anatarajia kujenga kanisa lake pia mwaka 2017 alitoa nyimbo yake kwa jina la Wapo ambayo ilimfanya akamatwe na polisi ila baada ya muda wa siku moja Rais wa Tanzania aliagiza Nay atolewe jela awe huru na kumuomba aongeze baadhi ya mashairi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *