Uncategorized

HUYU NDIYE B DOZEN NA MAPAMBANO YAKE YA KUFIKIA DREAM ZAKE ZA MAISHA.

on

“AMINI KWENYE NDOTO ZAKO” PHILOSOPHY OF B DOZEN

Unapotaja watangazaji bora hapa Tanzania katika upande wa burudani huwezi kumuacha B DOZEN. Anamiliki kampuni yake ya BORN TO SHINE  ambayo ni brand maarufu sana bongo. Ni kijana ambaye anakipaji kikubwa sana cha kutangaza na pia amewahamasisha vijana wengi sana kupenda kutangaza na inavyoonyesha kwa tasnia ya kutangaza kwa sasa watangazaji wengi wanamuiga sana katika style ya utangazaji.

Arusha ndiko ambako alianzia harakati zake za kuonyesha uwezo wake wa kutangaza. Alijiona anakipaji cha kutangaza pale ambapo alimuona mtangazaji JOHN DILINGA enzi hizo akitangaza tangazo ambalo lilikuwa likirushwa na kituo cha ITV.

Alimchukua msichana ambaye ni Binabu yake na kuamua kufanya hilo hilo  tangazo huku akimuiga John Dilinga katika hilo tangazo na walikuwa wakijirekodi na kuficha mkanda(tape) katika chumba chake. Siku moja mama alikuta hizo tape ndani ya chumba cha B DOZEN hapo ndio aligundua kwamba mwanaye anajua kutangaza.

Aliendelea kujirekodi na kumsikilizisha mama yake mara kwa mara na Mama yake hakuwahi kumatisha tamaa siku moja.

Alisikia kwamba CLOUDS FM wanafungua ofisi Arusha ndipo naye akajaribu kwenda kutafuta bahati yake hapo. Alikutana na mtangazaji anayeitwa DJ SUMMER D ndiye aliyejuwa anasimamia kituo na B Dozen alikutananae na kumwambia anakipaji cha kutanhaza jamaa alimponda sana ila mama alizidi mtia moyo.

                              Dozen na mtoto wake wa kiume

Mara ya pili alikutana na Mtangazaji GADNA G HABASHI  ya kumwambia anaweza tangaza Gadna alimpa nafasi ya kumwonyesha kipaji ila alimwambia analafudhi ya kichaga baada ya muda Gadna alienda Dar na pia CLOUDS iliungua na moto.

Gadna alirudi tena Arusha na Dozen alikutana nae tena hapo alipewa nafasi ya kutangaza katika  kipindi na kukabidhiwa kwa Glory Robson ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa REDIO FREE . Glory alimzingua Dozen kiasi kwamba Gadna alifungua mlango na kuja kisha akazima maiki na kumwambia Dozen arudi tena kwa ajili ya kufanya kipindi.

Hapo alifuzu na kuajiriwa rasmi ndani ya CLOUDS MEDIA na kufanya kipindi ambacho kina pendeka sana hapa Bongo XXL pia katika shoo ya FIESTA TOUR yeye ndiye coordinate wasanii wa ndani.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *