Uncategorized

HUU NDIO UTAJIRI WA KANYE WEST

on


Kanye went ni  producer, rapper, fashion designer na actor kutoka nchi ya Marekani, kutongana na mtandao wa celebrity net worth Rapper huyu mwenye miaka 38 kutoka Atlanta anautajiri wa kiasi cha dola milioni 145.

Kanye west ambaye aliamua kuacha shule akiwa collage na kuamua kufanya muziki kama kazi, alianza kwa kusainiwa katika record lebo ya Jay Z inayoitwa Roc-A-Fella Records kama rapper. baada ya hapo alifanikiwa kutoa albamu takribani saba ambazo ni kama vile “The College Dropout,Late Registration”, “Graduation”, “808s & Heartbreak”, “My Beautiful Dark Twisted Fantasy” ambazo zimefanikiwa kuwa ndani ya chati ya billiboard top 100 kwenye namba moja hadi kumi. Albumu hizi ziliuza sana duniani kwa mafanikio makubwa.

NI Mfanyabiashara anayemiliki Fatburger restaurants ambazo zinapatikana katika eneo la Chicago pia huwa anatengeneza viatu vya mpira katika kampuni ya nike vinavyoitwa air yeezy vilevile ana foundation yake ambayo husaidia watoto wa Africa, Amerika katika kuinua vipaji vyao.

Kanye West ameshinda tuzo 40 zikiwemo za  21 Grammys, saba BET awards, na mbili za  American Music Awards. Kanye kwa sasa amemuoa mwanamitindo Kim Kardashian na wana mtoto mmoja wa kike anayeitwa North West.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *