LifeStyle

Hizi ndizo tabia za kiongozi mbaya

on

Kuwashusha hadhi wafanyakazi wako.

Pale ambapo kiongozi anaona kampuni au Shirika anayoongoza mapato yanashuka badala ya kutafuta suluhisho anaanza kuoanisha kazi za sasa za  wafanyakazi wako ni sawa na walizozifanya zamani hivyo kuanza kutumia kauli chafu na kuwafananisha na hata viumbe bila kujua madhara yake ni kama kushusha morari ya wafanyakazi kutokana na matokeo haya. Tambua kazi ya kiongozi ni kupandisha hamasa kwa anaowaongoza pindi tatizo linapotokea.Kutokutoa picha nzima ya malengo

Kiongozi ambaye analeta mezani project fulani lakini anapotoa maelezo kwa wafanyakazi wake anashindwa kuwaambia kinagaubaga malengo na njia za kutekeleza project hiyo na kuwalazimisha wafanyakazi kutekeleza bila kujua madhara yake.Kutokukubaliana na juhudi za wafanyakazi

Pale ambapo wafanyakazi wako wanafanya project zako kwa umahiri mkubwa wewe kama kiongozi unaamua kutowapongeza na kuona ni kitu cha kawaida tuu, kisha wanavyozidi kuona wewe huoni juhudi zao wanaanza kukata tamaa na wewe na kuamua kupunguza juhudi hapo wewe unaamka na kuanza kuwa dharau hii itapelekea wewe kutokudumu na wafanyakazi mahiri.

Kiushindwa kuendesha jahazi

Viongozi wa aina hii ni wale ambao huchukulia kila kitu ni sawa pale ambapo mfanyakazi hafanyi vyema wewe unachukulia kawaida tuu, pale ambapo matokeo yanakuwa mabaya unanyamaza kimya tafsiri yake ni kwamba wewe ni kiongozi ambaye huongozi.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *