Health&Food

Hizi ndizo hatua nne(4) za uumwaji wa Ugonjwa wa UKIMWI/ AID’s

on

 

HIV ni kirusi ambacho hushambulia na kuharibu sehemu ya mwili ambayo huusika na upambanaji wa maradhi yaani mfumo wa kinga ya mwili hasa hasa hushambulia seli kuu mbili ambazo ni CD 4 Cells na Macrophages. Virusi hivi hushambulia na kuharibu seli hizi kisha kusababisha mwili kushindwa kupambana na vimelea vya Maradhi hivyo kupelekea kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.

hatua nne(4) za uumwaji wa Ugonjwa wa UKIMWI/ AIDS

1. Hatua ya awali

Katika hatua hii ambayo mtu huumwa mafua kwa muda wa wiki kadhaa pia asilimia 20% ya watu wengine wakiwa katika hii hatua humwa sana kiasi kwamba wanalazwa hosipitali ila wakipimwa virusi vya UKIMWI huonekana hawana maambukizi.

Katika hii hatua virus vya UKIMWI huwa vipo katika damu ambayo ipo katika mishipa ya damu ya mbali sana pamoja na mfumo wa kinga ya mwili vikiwa na kazi ya kutoa HIV  Antibodies ambazo zitakwenda kupambana na cells hai za mwili pia kutoa sumu ambayo itakwenda kupambana na mfumo wa kinga ya mwili. kitaamu kitendo hiki huitwa serology Conversation.

2. kutokea kwa dalili

Hii hatua inaweza kudumu kwa muda wa wastani wa miaka kumi pia mtu huwa haonyeshi zile dalili kali sana sana dalili ambazo huonekana ni kama kuvimba kwa tezi , kisha hapa mtu akipimwa damu ili kuchunguza kama ana virusi vya UKIMWI vipimo huonyesha damu yake inavirusi ya UKIMWI.


3. Dalili za maambukizi ya UKIMWI

Kwa muda mrefu mfumo wa kinga mwilini huaribiwa sana na virusi hivi hivyo kupelekea mambo yafuatayo;

 

  • Tezi na misuli ya mwili kuteketezwa
  • Kuzaliana sana kwa virusi ya UKIMWI hivyo kupelekea uangamizaji wa seli za CD 4
  • Mwili kushindwa kuzalisha tena CD 4 ambapo zimeangamizwa na virusi.

Dawa za kupunguza makali ya Virusi hivi huanzishwa kwa mgojwa katika hii hatua pindi ambapo CD 4 zake zinaonekana kupungua pia Magojwa nyemelezi huanza kumshambulia mwathirika wa UKIMWI. Karibia ya mifumo yote ya mwili huwa tayari imeshaashambuliwa na virusi hivi magojwa huzidi kuzidiwa sana.

4. Maendeleo kutoka kwenye Virusi ya ukimwi kisha kuwa Ukosefu wa Kinga Mwilini(UKIMWI)

Baada ya kinga ya mwili kuendelea kuharibiwa sana mwathirika hupata magojwa nyemelezi makili kama cancer hivyo huweza kukutwa na UKIMWI

Kwa watu wazima na watoto wa miaka 5 na zaidi CD 4 zao huwa 200cells/mm3 swa na asilimia 15 za CD 4. kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 CD 4 zao huwa chini ya asilimia 25. Vigezo vya kuchunguza UKIMWI hutofautiana kulingana na mwongozo wa nchi yenyewe.

KIINI
www.aids.org.za

Mtokambali 728x90

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *