Cellebs

Fahamu kiundani maisha ya msanii Rayvanny

on

 

Amezaliwa katika familia ya watoto nane na yeye ni mtoto wa mwisho katika Familia amezaliwa 1993 asili yake ni mtu wa Mbeya na familia yake karibia ya ndugu zake wote wanaishi huko tabora. Alianzia muziki katika kundi  la TipTop connection  na kutoa mpya ya kwake aliyoipa jina la “Mwenyewe” na haikufanya vizuri baada ya kuvurugana na meneja wake Bab Tale.
Alianza kurap baadaye alianza kuimba.

mwaka 2017 alifanikiwa kupata mtoto wa kiume na mpenzi wake aitwaye Fayma.

Yeye anasema moyo wake upo kwenye muziki kwa hiyo anafanya vyote. Muda mwingi huwa anafanya mazoezi ili kujiweka vizuri kimuziki. Amewahi kuwasaidia watu kimuziki studio kwa kuwatungia nyimbo.

Alikutana na Diamond baada ya Maromboso na Diamond kuwa studio na yeye alikuwepo, baad ya Diamond kuona Ray anachangia vizuri basi Diamond alimpenda na kuamua kufanya naye kazi. Akamkaribisha WCB na kurekodi nyimbo tatu na kuamua kuanza na “Kwetu” baada ya hapo aliamua kuwa chini ya label ya WCB.Anasema kwamba kwake Harmonize ni ndugu na ni rafiki yake sana na Diamond ni zaidi ya familia kwake.

Aliwahi kukaa mwenyewe na kuanza kulia kwa sababu watu walimdharau. Ndugu zake walimuona kama mla unga kwa sababu mziki ulikuwa haumtoi. Kwa sasa yuko kwenye hatua za mwisho kuona mafanikio ya kipaji chake kupitia nyimbo yake inayopingwa sana Tanzania nzima. Na kwa sasa ana nyimbo mpya aliyofanya na msanii mwenzake ambaye yuko chini ya label ya WCB Harmonize, nyimbo yao inaitwa “Penzi”

Baada ya kutoa ngoma yake ya Kwetu mwaka 2016 ilishika chati sana na kumtambulisha rasmi kwenye maisha ya muziki hata hivyo hakukawia aliachia ngoma nyingine inayoitwa natafuta Kiki kisha mwaka 2017 ametoa ngoma yake mpya Inayokwenda kwa jina la Zezeta pia mwaka 2017 ametajwa kuwania tuzo kubwa hapa Africa zinazotolewa na Mtvbase Africa.

Rayvanny amefanikiwa kushinda tuzo ya BET kama Best International viewers Choice ikiwa ni tuzo ya kwanza ya BET kuchukuliwa na msanii kutoka Tanzania.

Mtokambali 728x90

Recommended for you

2 Comments

 1. JOSUE MIRIMO

  November 1, 2017 at 4:22 am

  asante sana mimi ni JOSBUSARA nikiwa goma/DRC. sasa Ray vanny huku wanasema eti ni mdogo wake na diamond hiyo ni kweli?

  • Roman Olomy

   November 9, 2017 at 5:17 pm

   hayo maneno siyo ya kweli ndugu Josue Mirimo kutoka Goma|DRC msanii Rayvanny amezaliwa huko mbeya Tanzania na Diamonnd ni mzaliwa wa kigoma hao wanafanya kazi pamoja ila siyo ndugu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *