Inspiration

Hivi ndivyo watu wenye mafanikio hukabiliana na Matizo

on

 

1. Hufanya ni lakwao.

Usimnyooshee kidole mtu yeyote baada tatizo kutokea pokea kisha usitafute visingizio vya aina yeyote kabisa pia usijiameheshe mwenyewe lipokee hilo tatizo kisha tafuta namna ya kulitatua.

2. Huomba msamaha.

Tatizo lolote lile likitokea lazima lihusishe na rafiki zako au wafanyakazi wako hii ni kutokana kwamba tunaishi dunia kwa hiyo lazima tukutane na watu duniani cha msingi ni kujishusha na kuomba radhi wale wote walioathiriwa na tatizo lililotokea.

3. Hukubaliana na matokeo.

Kuomba msamaha bila kuwajibika katika tatizo lililotokea ni kitu kisicho na faida kwa hiyo unatakiwa kuongeza muda wa kufanya kazi au kugharamia hasara iliyopatikana ili kuhakikisha kwamba umeweza kusahihisha tatizo lililotokea.

4. Hujifunza kutokana na tatizo hilo.
Fikiria kwa makini chanzo kilichosababisha hilo tatizo kisha angalia lilivyotokea elewa kinagaubaga vitendo vilivyosababisha hilo tatizo kisha angalia hatua ulizochukua  weka lengo la kutorudia tena kwa sababu hii itakupa uzoefu kisha tumia huu uzoefu ili kuongeza ubora wako wa kutatua changamoto unazokutana nazo.

5. Huacha liende

Baada ya hayo kinachofuata ni kurudisha furaha yako na kufanya kazi kwa hali ambayo haonyeshi kwamba kuna kitu kimekutatiza katika hali yako..
Fanya haya na utaona jinsi utaenda vizuri.

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *