LifeStyle

Hivi ndivyo unaweza anzisha biashara yako hata kama mfukoni hakuna mtaji mkubwa.

on

1. Tengeneza kitu 
Je nini umefikiria ndio kinatakiwa kuwa kama biashara yako? kama una elfu hamsini na unahitaji kuwa na duka labda la nguo kubwa tuu ambalo unapanga gharama yake iwe ni milioni labda tatu. usikae chini ukisubiri milioni tatu ifikie ;jambo moja nunua ata nguo za mtumba za gharama ya elfu hamsini kisha anza kuuza kwa kutembeza au kwa namna ambayo unajua wewe au ni Unataka kufungua hoteli afu anza kama mama ntilie au baba ntilie faida yake ni watu watakutambua kisha watajua wewe unafanya nini pia mtaji wako utaanza kuongezeka kidogo kidogo cha zaidi sana utajua changamoto ambazo zinahusiana na ujasiriamali wako na kuzitatua kabla hujawekeza kiasi kikubwa cha pesa.


2. Uza kitu kwa mara ya pili 
Nunua kifaa kwenye maduka yawe ya rejareja au jumla nenda nacho hadi mtaa unaokaa tangazia  majirani au tumia mitandao ya kijamii kukitangaza anza na kimoja au viwili hakikisha hununui kingine kabla ya kununuliwa kile ulichonacho hii ni kuepesha hasara na msongamano wa vitu sehemu ambayo haiusiki. Muda mwingine chukua mahitaji ya watu au mtu anayehitaji kisha kanunue umletee hii itakuwezesha wewe kuwa na uhakika wa soko na kutopata hasara


3. Uza huduma yako
Usikae nyumbani na kusikitika kwamba huduma yako unayotaka kufanya kama malengo yako bado muda haujafikia toka nje fanya kwenda kuuza kuuza nguo au chakula  au chochote kile hii ni nzuri sana kwa sababu pengine wanaotoa huduma hii hawana fikra au njia nzuri za kutoa huduma unayotaka kwa hiyo pale utakapoanza tuu huenda ukavutiwa na watu wengi na kupata wateja wa kudumu.

4. Huduma zako toa kwa bei rahisi kwanza
Usiwe na tamaa ya pesa kitu cha kwanza kinachotakiwa kiwe katika akili yako ni kujulikana na kutengeneza jina hakikisha bidhaa zako wewe unazitoa kwa bei ambayo haiendani na ile ya wale wazoefu wa bidhaa hiyo lengo la hii mbinu ni kuleta wateja kutoka walipoweka mizizi na kuja kuweka mizizi kwako usitake faida kubwa mwanzoni fikiria wateja wengi na wakubwa mwanzoni.

Mwisho  hakikisha kwamba baada ya kusoma hapa unachukua hatua na kuanza kufanya kitu kuhusu ujasiriamali wako.

Recommended for you

2 Comments

 1. Herieth

  May 3, 2017 at 6:41 am

  Ushauri mzuri , Blog nzuri 📈

  • Roman Olomy

   May 6, 2017 at 9:12 am

   nashukuru sana, fanya iwe blog yako ya kutembelea mara kwa mara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *